Mwenye UKIMWI akitumia ARV hana tena uwezo wa kuambukiza wengine!

Asante sana kwa maelezo mazuri mshinga.
 
Mshinga,

Mkuu ningeanza kwa kusema, thread yako ni nzuri ukihitaji kuelimisha lakini baadhi ya vitu inaweza kuonekana inapotosha/kukanganya watu.

1 Thread title, yako ina TANGAZA (declare) kuwa, mtu aliyeathirika na VVU, akitumia dawa tajwa, hatasababisha maambukizi, kitu ambacho SI KWELI.

2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Muda toka mgonjwa kupata VVU?
-Muda toka mgonjwa kujitambua na kuanza kutumia dawa?
-Ni kwa muda gani muathirika amekuwa akitumia dawa?
-Muathirika amekuwa akitumiaje dawa?
-Uwepo wa magonjwa nyemelezi, na haki nyingine zenye kusababisha kinga mwili kuwa chini.

3. Kwa kuwa Tafiti ni nyingi, na ni kila leo, ingekuwa vyema ukituwekea hapa, au kuelezea ni Nani alifanya tafiti hizi, wapi na kwa muda gani!

4. Kama wadudu hufubazwa kama ulivyosema, kuna haja gani ya kutumia tena dawa, maana kinga mwili hutosha katika hatua hiyo.

5. Je, kutokana na thread hii, unachoweza kusema ni kuwa tukiondoa wagonjwa ambao hawajatambulika, Tanzania TUMETOKOMEZA UKIMWI? maana asilimia kubwa ya wagonjwa waliotambulika wanatumia dawa za kupunguza makali (ARV).. (By NHS under MoHSW ya October 2013)
 
Last edited by a moderator:
Vip kuhusu sis wa uvinza? hatari ya maambukiz ikoje?

inawezekana kuambukizwa kwa sababu huko nako kuna virusi na ikitokea una michubuko,japo kwa hapa sina details ni kwa kiasi gani ni hatari zaidi kufanya vile
 
asante mkuu kwa ufafanuz wako, swali langu nilikuwa nataka kujua kuhusu tohara kwa wanaume kuwa kunasaidia kupunguza maambukiz kutoka kwa mwanamke mwenye vvu kwenda kwa mwanaume ambaye hajaathirika. Hili limekaaje mkuu naomba ufafanuz wako.
tafiti zilizofanyika kufikia mwaka juzi zilionyesha kuwa mtu aliyetahiriwa ana uwepo mkubwa wa kujikinga na maambukizi, lakini kumekuwepo na maswali mengi yenye kutilia mashaka uwezo mkubwa ulitajwa kusaidia kujikinga na ukimwi,mfano AFRIKA KUSINI ndio nchi ambayo torara inafanyika kwa kiasi kikubwa karibu kuzizidi nchi zote za afrika lakini nchi hiyo hiyo ndiyo nchi yenye maambukizi makubwa kabisa barani afrika,nimekupa maelezo yote kutoa tahadhari kuwa ni kweli tafiti za awali zilionyesha tohara inaweza kukukinga na maambukizi ya ukimwi kwa asilimi nyingi lakini bado haijathibitika kabisa na tafiti zinaendelea kujua ukweli zaid na kukusanya takwimu
 
NIMEKUSOMA! Nina KAWAIDA YA KUFANYA MASTERBATIO KWA MUDA MREFU SANA EVEN MARA TATU PER DAY! Na NIKIMUONA DEM TU MZEE ANASIMAMA BALAA! Kuna athari gani za mastabeshn?


Ningependa niku saidie kukujuza kwa hilo
 
Nimependa hapo kwenye kupima wote,is the best way kwa watu wenye mahusiano.Hilo la mmoja kuwa nao na mwingine kutokuwa nao baada ya kuanza ARV nalo linaweza kuwa na ukweli fulani kwani nimeshakutana na kesi mbili za aina hiyo,ila hilo la kuwa Condom siyo reliable kwa kiwango ulichoeleza hapo juu nakuunga mkono for only 1%,nionavyo mimi ni vise versa.
 
Mshinga,

Mkuu ningeanza kwa kusema, thread yako ni nzuri ukihitaji kuelimisha lakini baadhi ya vitu inaweza kuonekana inapotosha/kukanganya watu.
asante kwa pongezi zako,thread haipotoshi ila inaweza kuwa inachanganya, na swala la kuchanganya lina sababu nyingi ikiwemo uelewa wa mtu mmojmoja,tafiti zenyewe zinatofautiana wakati mwingine.
na sayansi hupingwa ama kukubaliwa kupitia tafiti na si kitu cha ajabu katika tafiti kusema kuwa tafiti fulani haikuwa sahihi baada ya tafiti nyingine kutoa majibu tofauti, for instance the mississip person who was reported being treated from HIV came to be revealed he was not after a long time as he showed signs of HIV DNA japo hakuwa na virusi

1 Thread title, yako ina TANGAZA (declare) kuwa, mtu aliyeathirika na VVU, akitumia dawa tajwa, hatasababisha maambukizi, kitu ambacho SI KWELI.
si kweli,kwa mantiki ipi?ndani nimeeleza kwa maelezo marefu,kimahesabu asilimia 96 ni kama hakuna kabisa uwezekano na kisayansi hakuna kitu chenye ufanisi wa asilimia 100.

lakini hata hivyo nilifanya hivyo kuvuta wasomaji wengi kwa kuwa topiki nyingi za ukimwi hupuuzwa tu, na hata hii mpaka sasa wameisoma wengi tofauti na topiki nyingi za ukimwi

2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Muda toka mgonjwa kupata VVU?
hapa sijakupata hasa swali lako lililenga nini,lakini ngoja nijitahidi kujibu,mtu ninaemuongelea ni yule anaetumia ARV, matumizi ya ARV hayaamuliwi kwa muda bali yanaamuliwa kwa kiwango cha CD4 kilichobakia kwenye mwili wa mtu,na CD4 zikiwa chini ya 350 ndio mgonjwa anaruhusiwa kuanza kutumia ARV lakini hapo kabla alikuwa hatumii na kama alikuwa hatumii maana yake ana uwezo mkubwa wa kuambukiza wengine


2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Muda toka mgonjwa kujitambua na kuanza kutumia dawa?
kujitambua tu kwa mgonjwa haimfanyi aanze kutumia ARV,bali ni mpaka vigezo vya kutumia ARV awe ametimiza,nadhani nimeeleza hapo juu japo kwa ufupi

2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Ni kwa muda gani muathirika amekuwa akitumia dawa?
muda hautajwi kwa maana ya kwamba inahitaji labda wiki kadhaa,lakini imeelezwa tu kwamba kwa mtu anaetumia ARV na nina uhakika watu waliofanyiwa utafiti watakuwa ni wale waliokuwa wanatumia muda wote maana kwenye tafiti lazima kuwe na watu wanaokuwa monitored

2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Muathirika amekuwa akitumiaje dawa?
mashariti ya kutumia dawa yanafanana,na ukikiuka ni tatizo jingine,lakini matumizi ya zile dawa ni kila siku na hilo ndilo sharit kuu ambalo kila mtu anatakiwa alifate na hivyo ndivyo namna ya kuvitumia vidonge na si vinginevyo

2.Hii inazua maswali mengine, ni muda gani unaongelewa hapa, yaani
-Uwepo wa magonjwa nyemelezi, na haki nyingine zenye kusababisha kinga mwili kuwa chini.
magonjwa nyemelezi kwa sasa hayapo,kama mtu akipima mapema na ikaonekana CD4 zake ziko zaidi ya 350 huyo hupewa dawa nyingine baada tu ya CD4 zake kuonekana kuwa ni zaidi ya 350 na dawa hizo kazi yake ni kuzuia magonjwa yote nyemelezi, na ndio mana siku hizi si rahisi kumuona mtu ana magonjwa nyemelezi kwa kuwa wanapewa dawa ya kuzuia magonjwa nyemelezi



lakini kwa wale ambao hawapimi na kupewa vidonge vya kuzuia magonjwa nyemelezi ndio unaweza kuwakuta wanapata hayo magonjwa.

kinga kuwa chini inatokana na kushambuliwa kwa seli na HIV

3. Kwa kuwa Tafiti ni nyingi, na ni kila leo, ingekuwa vyema ukituwekea hapa, au kuelezea ni Nani alifanya tafiti hizi, wapi na kwa muda gani!
maelezo yangu yanajumuisha tafiti nyingi na zingine nimezisoma zaidi ya mwaka mmoja, na hivyo ningetaka kuzileta kama zilivyo wala topic isingekuwa hii na maelezo yasingekuwa haya maana kila utafiti unakitu unachokisimamia na maelezo yake ni ya kitaalamu zaidi na wengi si rahisi kuyaelewa na waishia kuelewa kina nyinyi na mimi tu,mimi nimejitahidi kutoa ufupisho wa maelezo kwa mjumuiko, pia najua shida kubwa ya language barrier kwa watu wengi na ndio maana sikutaka kuweka maelezo kama yalivyo maana watu ambao wangeelewa na kufaidi ni wachache zaidi,na staili hiyo huwa siipendi maana kila swali la mtu ningekuwa naleta maelezo yote ya kiingereza hapa bila kujali uwezo wa kiingereza wa muuliza swali,

hapa nimewafanya watu wengi kuelewa nilichokiandika maana hata kama watu hawapendi ukweli lakini nasema kiingereza ni tatizo hata kwa waliosoma na wana degree na hata masters. na ndio maana nimejitahidi sana kuandika kwa kiswahili karibu kila sehemu ila niliposhindwa kabisa kutoa tafsri ndio nimetumia maneno ya kiingereza.

binafsi huwa natumiwa email za tafiti mbalimbali kutoka aidsmap.com ya uingereza kila wiki na ni bure na tafiti hizo ni za sehemu mbalimbali za dunia. unaweza kutembelea.

pia huwa nasoma kutoka sehemu zingine mbalimbali



4. Kama wadudu hufubazwa kama ulivyosema, kuna haja gani ya kutumia tena dawa, maana kinga mwili hutosha katika hatua hiyo.
kuvifubaza virusi ni kazi ya kila siku na ni sawa na kuvipa vidonge vya usingizi na ukiacha kesho kuvipa vidonge vya usingizi basi vinaamka tena na kuendelea na kazi zake kama kawaida,kwa hiyo havifubai milele,dawa ya kila siku ndio inavifanya visiweze kufanya lolote na punde ukiacha vinaamka na kitu kibaya zaidi ni kwamba vikiamka vinajenga usugu kwa dawa na vinakuwa very restive than before.

UKIMWI haujatokomea upo tena sana na maambukizi ni makubwa, sema athari nyingi za UKIMWI hasa kwa wagonjwa wenyewe zimepunguzwa sana
 

mkuu asilimia 70% kwa kondomu ni kubwa sana na inatosha kabisa kuzuia ukimwi, na kitu kinachopunguza asilimia za kondomu ni kuwa matumizi yake ndio changamoto kwa wengi lakini nayo ikitumiwa kwa usahihi zaidi ina zaidi ya asilimia 70 kuzuia maambukizi
 
Ningependa niku saidie kukujuza kwa hilo

nami nasema msaidie mana hapa si mtaalamu sana,specific nimesoma tu tafiti nyingi za ukimwi na wala udakitari si taaluma yangu, na biology yangu ni ile ya fm4
 
Chief Unaweza kutoka link ya reference ya study zilizofanyika pili kuondoa doubt kwa wengi? Binafsi hii ni habari mpya kwa 100%
 
Hapo umenena mkuu,matumizi sahihi ya condom nalo ni tatizo,inaweza kuwa ni uelewa mdogo au mchecheto ukishaona yale mambo yetu!
 
Mshinga, Hapa ndipo ninaposema kunapokuwa kuna UPOTOSHAJI.

1. Kisayansi, Hatuvutii watu kusoma, bali ukweli ndio unaoongea...Mada kutopendwa haimaanishi UVUTIE KWA KUPINDISHA UKWELI, to make it palatable to some people DOESN'T MAKE IT TRUE, mkuu.

2. Usemapo atumiaye dawa za ARV haambukizi virusi, na kisha kusema kwa asilimia chache bado inaleta MKANGANYIKO, na ndio maana hapa nikasema hebu na tuone statistics za wapi, na study hii ilifanywaje, zisije kuwa study za mtu mmoja , under sample size ya watu thelathini, then tuhitimishe kwa kusema hayo hapo juu.
Pili, dara validation ina umuhimu wake, tafiti zinapofanyika hutoa asilimia fulani kwa maana ya majibu, mfano confidence values/interval na hapa ndipo kwenye uzito wenyewe.

3. Uliposema hujaelewa, nikufafanulie..Unasema kuwa mgonjwa/muathirika akitumia ARV huwa katika hali ya kutoambukiza, nami nikauliza unapoongelea suala la utumiaji wa ARV na "kutosababisha maambukizi" unapaswa kutambua muda.
-Hapa namaanisha Muda wa Utumiaji dawa. Mf. magonjwa hutofautiana, na hata uwepo wa dawa katika mwili/mzunguko wa damu (Half life) hutofautiana.Yaani mgonjwa anapotumia dawa za malaria, si sawa na dawa za Kichocho.
Sasa unapokuja katika suala la UKIMWI picha ni tofauti, kwa sababu kitabibu kuna vitu viamuavyo/viashiriavyo hali ya uponaji wa mgonjwa kama.(Prognostic factors)

i. Muda wa mgonjwa kujitambua hadi kuanza kutumia dawa.
(aliyeathirika toka mwaka 1999 na kuanza kutumia dawa mwaka 2013 si sawa na aliyeathirika mwaka 1999 na kuanza kutumia dawa mwaka 2000)

ii. Muda mgonjwa aliyowisha tumia tiba.( Hapa namaanisha Muathirika aliyetumia dawa kwa Mwaka mmoja si sawa na aliyeanza kutumia dawa wiki mbili, ingawa wote ni waathirika).

iii.Muathirika amekuwa akitumiaje dawa.
Hapa, kuna mengi sana ya kuongelewa, mara kadhaa wagonjwa huacha dawa wanapojisikia unafuu/au hali fulani ya kumudu kazi zao za kila siku. Pili kuna kipindi cha nyuma dawa zilikuwa za shida katika baadhi ya vituo hivyo kufanya kutopatikana kwa urahisi. Tatu, kutokana na baadhi ya madhara mfano, Ganzi, kuishiwa damu n.k waathirika wamekuwa wakisita kuzitumia.Sasa uwapo na wagonjwa wawili mmoja mwenye kutumia dawa kila siku na mwingine mwenye kuwa katika tiba anapojisikia, ni yupi mwenye kusema "hawezi kuambukiza"..au kwako wote hawa ni sawa?!!!
Ikumbukwe tunapoangalia Clinical, Immunological treatment faiure, IRIS, n k muda kama ambavyo nimekwisha sema hapo juu ni crucial.

4. Ninapingana na wewe kusema kwamba maginjwa nyemelezi hayapo, mkuu sijui uko maeneo gani au labda hospitali/ kituo gani cha afya ambako hakuna wagonjwa hawa! Lakini kwa uelewa wangu mdogo, ni kwamba magonjwa nyemelezi yapo sana, na hata kwa baadhi ya wagonjwa ambao wamekuwa wakitumia kinga (CTX prophylaxis).
Ikumbukwe, kuwa si vituo vyote vyenye dawa, si waathirika wite watumiao dawa inavyopaswa, si waathirika wote wenye kujijua!

5. Mwisho mkuu, tafiti ni nyingi, na ni vizuri kupata taarifa kupitia barua pepe kama ambavyo umesema hapo juu, Subsription ni jambo ambalo mtu yeyote anaweza kufanya na kupata taarifa hizo, ila cha muhimu ni VALIDITY ya taarifa. Muda wa tafiti zaidi ya mwaka mmoja ni mwanya/pengo kubwa kitabibu hasa kitafiti! Mfano tazama baadhi ya takwimu niliyoweka ya miezi miwili iliyopita ina tofauti kubwa na maelezo yako.
 
Last edited by a moderator:

Nilitaka kujua kati ya mwanaume na mwanamke nani mwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nikupe pongezi kwa maelezo yako mazuri na yenyekuhamasisha watu kuyasoma. Ila nami ningependa kuchangia mambo mawili matatu hivi ili kuuboresha Uzi huu

kwa kuwa umekiri mwenyewe kuwa we si daktari wa magonjwa ya binadamu pengine ni mwanaharakati wa mambo ya UKIMWI au muelimishaji rika tu, sasa nafikiri it's a right time ukaupload hapa hiyo paper ya tafiti unayorelay upon ili nasi tujiridhishe VALIDITY yake nafikiri utetezi wa kuwa unatumia tu via email au kutaja tu website hautoshelezi kudhibitisha maelezo.
Elewe mkuu sio ka tunakupinga na maelezo yako mazuri na yenyekuleta tumaini na faraja kwa watanzania wengi la-hasha ni katika hali ya kujiridhisha behind reasonable doubt maana hapa tunaongelea uhai wa mwanadamu.
Maambukizi yakishatokea there's no reverse mechanism kwahiyo tuwe makini jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…