Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

April 21, 2020
Kisaki Morogoro vijijini
Tanzania

MAGARI YAKWAMA ZAIDI YA SIKU TATU BARABARA YA MOROGORO KISAKI, TANROADS WALAUMIWA
Barabara iendayo Stiegler's Gorge katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project ( JNHPP) ipo katika hali mbaya amethibitisha Bi. Ruth John ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) alipokuwa akihojiwa toka eneo la mkwamo wa usafiri uliosababishwa na barabara mbovu huku malori ya mizigo kuelekea mradi mkubwa wa umeme na mabasi pamoja na magari mengine yakishindwa kuendelea na safari kwa siku kadhaa. DAS Ruth John ameilaumu watu wa mradi wa Stiegler's Gorge na TANROADS kushindwa wajibu wao ambao upo ndani ya makubaliano kukarabati barabara hiyo iendayo ktk mradi huo mkubwa wa umeme.



Pia Eneo la Kirengezi Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro magari yamekwama kwa zaidi ya masaa tano na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii jambo ambalo linawasukuma wananchi kuiomba serikali kujenga barabara kwa kiwango cha lami ili kuepukana na usumbufu unaojitokeza mara kwa mara hasa nyakati za masika.
Source: Kayuni Online TV
 
April 19, 2020
Mbweni, Dar es Salaam
Tanzania

Miundombinu ya maji ya mvua, majitaka na uwezekano wa kuchimba au kujenga canals na kingo za mito jijini Dar es Salaam
Source : Global TV online


April 25, 2020
Mbweni, Dar es Salaam

DC CHONGOLO ATINGA NA MITAMBO YAKE KWA BRIGEDIA MSTAAFU KUTATUA KERO YA MAFURIKO


Baada ya Global Tv kutoa taarifa ya Zaidi ya familia 50 zipatazo hamsini eneo la Mbweni Teta ,jijini Dar es Salaam zilizokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Chongolo, amefika katika eneo la tukio na mitambo maalumu kwaajili yakutatua kadhia hiyo ambayo imekuwa ikiwatesa wakazi hao tangu mwaka 2016...

Source : Global TV online
 
April 28, 2020
Mbeya, Tanzania

MAFURIKO YAKATA BARABARA YA MBEYA, CHUNYA TABORA DC. ATOA NENO



Mkuu wa wilaya ya Chunya, mhandisi Bi. Maryprisca Mahundi amefika sehemu ya daraja hilo muhimu la Bitimanyanga linalounganisha mikoa ya Mbeya, Rukwa, Tabora , Singida Mwanza kwa barabara na kutoa salamu za mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Albert Chalamila.

Abiria watoa rai kwa serikali kuipa kipaumbele barabara hiyo muhimu inayounganisha mikoa mingi ya Tanzania. Naye meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya amesema mkandarasi ana mobilize mitambo ili kurekebisha eneo hilo la daraja na barabara.

Source: MbeyaYetuOnline TV
 
Utasababisha watu wapitiloze lkati ya pori wakajikalie kwa kagame
 
May 4, 2020
Dar-es_salaam, Tanzania

Nyumba 350 Dar es Salaam maji yafika kina cha magotini, sasa wakaazi wanaishi na samaki ktk nyumba zao



Miundo mbinu ya barabara na mifereji iliyojengwa na serikali bila uchambuzi yakinifu ktk vitongoji vya Tungi, Visiwani, Machava yasababisha mafuriko eneo la Magogoni wilaya ya Kigamboni mkoa wa Dar-es-Salaam. Pamoja na wananchi kufanya harambee ya kukodi Excavator bado tatizo hilo limewashinda kuondosha maji hayo na kulia kuomba msaada toka serikali ya wilaya ya Kigamboni na ya Mkoa. Hali ni mbaya wananchi wanaishi na samaki aina ya perege na vyoo vimefurika na kuna hatari ya magonjwa ya kuharisha kuwakumba wakaazi wa eneo hilo.

Source : ITV Tanzania
 
Tuliambiwa SGR Dar to Morogoro ingeanza Dec mwaka jana, Stiegler's Gorge nayo kimya. Sio Msemaji wa serikali wala Polepole wala praise team wanaogusia, nini kimewapata.

Bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Tanga lilizinduliwa kwa mbwembwe tukaonywa atakayekwamisha atakiona, nani sasa amekwamisha. Je ule wimbo wetu wa kuhamia Dodoma umeishia wapi?

Tanzania ya viwanda imefikia wapi, juzi tuliambiwa tuna viwanda vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana, sijui hivyo vidogo sana ni vya wachoma mahindi?

Ndege zetu zimepaki? yaani.

Mambo ni mengi sana muda hautoshi.
Kama biashara ya makinikia. Vinaishia hewani tu. Hakuna jipya.
 
Mkuu viwanda gani unataka wakati huu tunazalisha barakoa zetu wenyewe na vyerehani vyetu
 
May 5, 2020
Dar-Es-Salaam, Tanzania

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dsm alonga

Kufuatia mafuriko na vilio vya wananchi mkuu wa wilaya ya Kigamboni Bi. Sarah Msafiri awatembelea wananchi na kutoa neno



Source : ITV Tanzania
 
May 7, 2020
Mkuraga, Pwani
Tanzania

Barabara mbovu, mbunge Abdallah Ulega aomba subira


Kufuati miundombinu mibovu ya barabara vijijini, Mbunge Abdallah Ulega (CCM) ambaye ni Waziri mdogo wa Mifugo ktk serikali, awaomba wananchi kuwa na subira baada ya kuona jinsi barabara zilivyo katika hali mbaya sana na kuwaahidi nguzo za umeme pamoja na nishati ya umeme zitafikishwa hivi karibuni.

Source : ITV Tanzania
 
May 8, 2020
Dodoma, Tanzania

TRENI YA UMEME TANZANIA KUANZA SAFARI HIVI KARIBUNI, WAZIRI ATHIBITISHA - "KENYA HAWAJAFIKIRIA"


BAJETI ya makadirio ya wizara ya Nishati, imeanza kujadiliwa Bungeni leo Mei 08, baada ya waziri mwenye dhamana, Dkt Medard Kalemani, kuiwasilisha Bungeni hapo.

Source: Global TV online
 
2396378_EA0E49A5-F5E2-46EE-9B1B-5E6806D1A6C4.jpeg

Picha njia ya juu ya reli ya SGR (viaduct) jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Hii picha ya front page leo 11/5/2020, Daily News gazeti rasmi la serikali ya Tanzania imenifikirisha sana
 
Kodi ya Maboresho na ujenzi wa reli ya SGR inatuhusu, hii ni ile inaitwa ' tunajenga reli kwa fedha za ndani'

https://taxsummaries.pwc.com › oth...
Tanzania - Corporate - Other taxes - Worldwide Tax Summaries

22 Nov 2019 · Most imports are also subject to Railway Development Levy of 1.5% (except goods that .

More info :
Tanzania to tax imports to finance rail projects :
Tanzania has instituted a 1.5 percent levy on all imports to fund rail projects intended to bolster national and international connectivity.

The new tax, based on the price, insurance and transportation of imports, will help the country raise $14.2 billion for rail projects.

One railway, at a cost $7.6 billion and length of 1,591 miles, will connect the country’s largest container port in Dar es Salaam with the landlocked countries of Rwanda and Burundi.

In 2012 and 2013, both countries posted economic growth above 4 percent, according to the World Bank. Growth in 2014 is also expected to exceed 4 percent.

The southern Tanzanian Port of Mtwara will also gain a hinterland 621-mile rail link to the country’s interior at a cost of $1.4 billion.

The remaining $5.2 billion set aside for rail projects will be used to modernize existing rail infrastructure as the country seeks to compete with Kenya for cargo bound for the African interior.

Tanzania imported 7,600 TEUs from the U.S. in 2014, and exported 1,500, according PIERS, a sister product of JOC.com within IHS Maritime & Trade.

The U.S.-Tanzania ocean container trade is dominated by the 2M Alliance, whose members Maersk Line and Mediterranean Shipping Co. carry 73 percent of the trade.

Source : Tanzania to tax imports to finance rail projects | JOC.com
 
May 5, 2020
Dar-Es-Salaam, Tanzania

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dsm alonga

Kufuatia mafuriko na vilio vya wananchi mkuu wa wilaya ya Kigamboni Bi. Sarah Msafiri awatembelea wananchi na kutoa neno



Source : ITV Tanzania

Dah hayo mambo kumbe yapo....Mimi huwa naangaliaga TBC tu kila kitu safi nchini
 
May 23, 2020
Kibaha, Pwani

Changamoto ya barabara Tanzania ya viwanda



Kata ya Visiga Zegeleni mjini Kibaha mkoa wa Pwani ina viwanda vingi lakini miundo-mbinu ya barabara kuelekea eneo hilo la viwanda imekufa na hali hiyo hujitokeza kila msimu wa masika na hapa ni mjini pia karibu na Jiji la Dar es Salaam

Source : Millard Ayo
 
31 December 2020
Mbeya, Tanzania

Waziri akumbana na barabara mbovu Busekelo Rungwe

Viongozi wa CCM ngazi za wilaya, vijiji na kata walilia barabara hiyo ya kilometa 28 iliyo mbovu inayoiunganisha Busekelo na Mbeya pamoja na maeneo mengine ya Tanzania. Ni barabara muhimu kwenda kwenye chanzo maji Mbeya lakini TARURA inayohusika na barabara hiyo bado hawajaifanyia kazi
Source : MbeyaYetuOnlineTv
 
Wamebaki wenyewe CCM Mpya sasa hawana kisingizio kuwa kuna upinzani "unachelewesha" maendeleo kote Tanzania pamoja na hii barabara ya Busekelo, Rungwe mkoani Mbeya.
 
Miradi yenyewe tunasaidiwa na serikali zingine lakini tunajipiga kifua binafsi kama vile tumeifanya wenyewe. Miradi ya kawaida tu lakin mbwembwe nyingi, waafrika bana tunashida sana, kila kitu siasa tu. Badala mjisifie kwenye sera zenye tija mnajisifia kwenye barabara... Poor creatures
 
Back
Top Bottom