April 21, 2020
Kisaki Morogoro vijijini
Tanzania
MAGARI YAKWAMA ZAIDI YA SIKU TATU BARABARA YA MOROGORO KISAKI, TANROADS WALAUMIWA
Barabara iendayo Stiegler's Gorge katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project ( JNHPP) ipo katika hali mbaya amethibitisha Bi. Ruth John ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) alipokuwa akihojiwa toka eneo la mkwamo wa usafiri uliosababishwa na barabara mbovu huku malori ya mizigo kuelekea mradi mkubwa wa umeme na mabasi pamoja na magari mengine yakishindwa kuendelea na safari kwa siku kadhaa. DAS Ruth John ameilaumu watu wa mradi wa Stiegler's Gorge na TANROADS kushindwa wajibu wao ambao upo ndani ya makubaliano kukarabati barabara hiyo iendayo ktk mradi huo mkubwa wa umeme.
Pia Eneo la Kirengezi Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro magari yamekwama kwa zaidi ya masaa tano na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii jambo ambalo linawasukuma wananchi kuiomba serikali kujenga barabara kwa kiwango cha lami ili kuepukana na usumbufu unaojitokeza mara kwa mara hasa nyakati za masika.
Source: Kayuni Online TV