Hbr wanajamvi ningependa kufahamu kutoka kwenu wanajamvi kuhusiana na hii taasisi inayoitwa baypot kuhusu utoaji wao wa mkopo baada ya kukamilisha vigezo vyote mikopo yao inachukuwa siku ngapi hadi unapata mkopo na je?hawa watu si wababaishaji vipi kuhusiana na rushwa
Hapana siyo wababaishaji ni baada ya Siku 2 hadi 3 unapata mkopo.Ila tatizo lao ni riba kubwa sana unalipa marejesho hadi mara 3 ya ulichokopa.Kwa hiyo haina msaada.
Usijaribu tafadhali utapata matatizo makubwa, narudia tena utapata matatizo makubwa sanaaaa..... Labda kama tu unataka kuacha kazi na kuhama nchi. ACHANA NA BAYPORT!
Nilifanya kazi hapo miez kadhaa, nikaacha baada ya kuona ntapata dhambi za bure, waliokopa wengi wanalia, mkopo utapata ndani ya masaa 24 lakin utajuta kwa miaka 5