Mwenye uzoefu na Majiko ya Induction ya ECOA anipe uzoefu tafadhali!

Mwenye uzoefu na Majiko ya Induction ya ECOA anipe uzoefu tafadhali!

kiukweli mimi siyatumii ila bibi yangu ndio anatumia sidhani kama analipikia ugali maana si ya kioo kwa juu? ila kama unapika ugali kuna ulazima gani wa kuyakandamiza?
Hapo nimekupata mkubwa.
 
Majiko haya ya inductor ni mazuri mm nilinunua mda kutoka home base asilimia 98 % natumia umeme kupika na nimeona unafuu mkubwa sana mkaa nilishasahau labda uwa natumia kulelea vifaranga , ges ipo kama backup mtungi mdogo wa kilo 6 namaliza nao mwaka .
 
kiukweli mimi siyatumii ila bibi yangu ndio anatumia sidhani kama analipikia ugali maana si ya kioo kwa juu? ila kama unapika ugali kuna ulazima gani wa kuyakandamiza?
Sio kioo kama hii glass ya kawaida yle ni material ya ceramic glass inahimiri joto la aina yoyote
 
Faida za induction cooker
1. Huivisha haraka
Joto huenda moja kwa moja kwenye sufuria, hivyo chakula huiva kwa muda mfupi.

2. Huokoa umeme
Nishati nyingi hutumika kupasha sufuria moja kwa moja badala ya kupotea kwenye mazingira. Tofauti na majiko ya infrared

3. Salama zaidi
Uso wa jiko haupati moto sana kama majiko ya kawaida.
Hakuna mwali wa moto kama kwenye gesi. Majiko mengi hujizima yenyewe sufuria ikiondolewa.

4. Rahisi kusafisha
Uso wake ni laini wa ceramic glass, hivyo uchafu na mafuta huondolewa kwa urahisi.

5. Udhibiti sahihi wa joto
Unaweza kuongeza au kupunguza joto kwa usahihi mkubwa wakati wa kupika.

6. Hupunguza joto jikoni
Kwa kuwa joto huzalishwa zaidi kwenye sufuria, mazingira ya jikoni hayapati joto kupita kiasi.
 
Hasara chache za induction cooker

1. Yanahitaji vyombo kama masufuria na frying pain vinavyokubali induction (vyenye kuvutwa na sumaku)

2. Bei ya ununuzi inaweza kuwa juu kuliko baadhi ya majiko ya kawaida

3. Yanategemea umeme; ukikatika huwezi kupika
 
Uimara wa jiko la induction kwa kawaida ni mzuri sana likitumiwa na kutunzwa vizuri.

Ceramic glass ya juu imeundwa kustahimili joto kubwa na matumizi ya kila siku.

Sehemu nyingi za jiko hazichakai haraka kwa sababu halina mwali wa moto wala vipengele vya kupasha joto vinavyoonekana wazi.

Majiko bora yanaweza kudumu miaka 8–15 au zaidi, kutegemea ubora wa bidhaa na matumizi.

Ili kuongeza uimara:
​
  • Tumia sufuria zenye sehemu ya chini iliyo tambarare.​
  • Epuka kuangusha vyombo vizito kwenye glass.​
  • Safisha kwa vitambaa laini na visafishaji vinavyofaa.​
  • Linda jiko dhidi ya mabadiliko makubwa ya umeme kwa kutumia kinga ya umeme (surge protector) ikiwa eneo lako lina hitilafu za umeme mara kwa mara.​
Kwa ujumla, jiko la induction la ubora mzuri ni imara na linaweza kudumu kwa miaka mingi likitunzwa vizuri.​
 
How do i know that?
Kifaa chochote cha umeme huwa wanaweka matumizi yake ya umeme kwa saa mfano unaweza ukaona kimeandikwa 1000w, 2000w n.k

Mfano ina maana gani kifaa cha umeme kikindikwa 1000w? Ina maana kinatumia unit 1 kwa saa au kitaalamu tunasema 1kWh. Ukitumia dakika 30 ni 0.5 kWh

Ikiwa jiko lako la induction limendikwa 2000w ina maana ukilitumia kwa saa 1 ni unit 2 za umeme (2 kWh)

Ndio maana inshauriwa mara zote unaponunua kifaa cha umeme kama hizi home appliances soma matumizi yake ya umeme yapoje
 
Kwa hiyo hayo ya induction yanatumia umeme kiasi gani kwa wastani?
 
Kwa hiyo hayo ya induction yanatumia umeme kiasi gani kwa wastani?
Induction kama ya ECOA ni 2000w hivyo unit 2 kwa saa. Makadirio ni kama ifuatavyo:

downloadfile-1.jpg
 
Induction kama ya ECOA ni 2000w hivyo unit 2 kwa saa. Makadirio ni kama ifuatavyo:

View attachment 3612811
Pia uzuri wa majiko ya ECOA unatumia App ya simu kwaajili ya kuangalia matumizi yako ya kila siku. Wanakuunganishia moja kwa moja kwenye simu yako kwaajili ya kufuatilia matumizi yake. So far ni jiko zuri na matumizi yake ya umeme ni kidogo mno. Mimi pia nalitumia kama Main jiko na Gas ni kama backup
 
Attachments

  • Screenshot_20260622_080517.jpg
    Screenshot_20260622_080517.jpg
    127.7 KB · Views: 10
Pia uzuri wa majiko ya ECOA unatumia App ya simu kwaajili ya kuangalia matumizi yako ya kila siku. Wanakuunganishia moja kwa moja kwenye simu yako kwaajili ya kufuatilia matumizi yake. So far ni jiko zuri na matumizi yake ya umeme ni kidogo mno. Mimi pia nalitumia kama Main jiko na Gas ni kama backup
Safi saana
 
Back
Top Bottom