Mwenye uzoefu wa gari za Byd yangwang kutoka China

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Gari za byd yangwang zinazotengenezwa china mwenye kujua zipoje.je kwa afrika zinafaa maana wanateknolojia ya umeme na smart AI nyingi sana kwenye gari.

Sifa ya injini yake inajitengenezea yenyewe umeme na kusukuma gari sio kama ile ya tesla mpaka uchaji ukilinginisha hii gari.

 
Broh, hongera kwa kufikiria kuhusu Electrical Vehicle (EV). Najua inaweza isiwe leo, ila miaka inayokuja tutajazana wote kwenye Hybrids, Plug-in Hybrids na Full EV. Running costs ni ndogo sana. Challenge kwa sasa ni purchasing costs na installation ya charging systems nyumbani.

Turudi kwenye topic.

Hao jamaa Yangwang ni brand ya magari luxury ya kichina inayomilikiwa na BYD Auto, ambao wana vyuma vikali hao BYD Auto mfano BYD Seal ambayo ukiiangalia unasema Tesla hii hapa.


Kwahiyo in summary, hao BYD Auto wana sub brands kama tatu moja wapo ndio iyo Yangwang, nyingine ni Denza na nyingine Fangchengbao.

Niliwahi tembelea kiwanda chao kimoja kulikua na maonesho aisee, Bongo tunakosa vitu vitamu sana.

Sasa ukirudi kwenye sub brand yako, ya Yangwang, hii kidogo ni mpya wameanza toa magari 2003 na wana model tatu tu.
Wana Yangwang U7 (hii ni luxury sedan), wana U8 (hii ni SUV ndio uliyoipost boss) na wana U9 hii ni supercar.

Hii U9 aisee ebu tuiangalie tumeze maji tulale. $230,000/= only.



Kwahiyo, challenge za kununua hizi gari sasa hivi ni gharama kubwa sana (nyingi mil 100 kwemda mbele), na challenge ya mafundi itakua ipo pia.
 
Niliwahi tembelea kiwanda chao kimoja kulikua na maonesho aisee, "Bongo tunakosa vitu vitamu sana". Tuache uchawa tufanyekazi za maana kama hizi, tutengeneze zetu badala ya kushinda Lumumba na kupiga domokaya. Mchina miaka ya 1970 hakutofautiana sana na sisi zaidi ya kuwa wao hawana vikundi vya domokaya, leo haooo! Ila mama kaupiga mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…