Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo Maswa mkoani Simiyu,Carolina Shayo amezuia mzabuni ya uondoshaji wa taka katika mji wa Maswa kutoendelea na kazi na hivyo kusababisha mji kuwa mchafu kila kona.
Ametumia vibaya madaraka yake kuzuia shughuli halali za serikali kufanyika baada ya mzabuni huyo kufunga mkataba na Halmashauri ya wilaya ya Maswa ambao ndiyo wanailea mamlaka hiyo.
Mamlaka hiyo inayoundwa na wenyeviti wa vitongoji ambao wote ni CCM wamefikia hadi hatua ya kumdhalilisha kwa maneno Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Maswa ya kumchafua katika jamii ili aonekane hafai.
CCM mkoa wa Simiyu wanalijua jambo hili lakini wapo kimya tu,Ofisi ya DC Maswa inajua jambo hili wako kimya,Vyombo vya ulinzi vinajua jambk hili lakini wako kimyaaa.
Soma Pia: Wenyeviti wa vitongoji mjini Maswa wamgomea Dc
Mji wa Maswa sasa ni mchafu kila kona na viongozi wa serikali wapo haqachukui hatua.
Hii Mamlaka inatakiwa kufutwa maana imeshindwa kufikia malengo kwa zaidi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwani imeshindwa kufikia malengo ya kuwa Halmashauri ya mji.
Tamisemi itupie macho suala hili ambalo ni muhimu kwa afya za wananchi na wakazi wa mji wa Maswa.