Miaka ya nyuma kidogo nilikwenda Tanesco wakati bado wapo pale ntuma ya samora avenue station au kama unaenda Police central, nilikwenda kumuona ofisa mmoja kwa ajili ya kunifungia Luku nyumbani.
Mule ofisini nilimkuta waziri wa nishati na madini Daniel Yona kabla hajapewa wizara ya Fedha, kwamba yeye ndio Boss wa Tanesco, na pale alukwenda personal kwa issue za umeme nyumbani au kwenye nyumba alizokuwa anajenga.
Baada ya Daniel Yona kutoka tu kwenye ile ofisi niliingia mimi na yule ofisa akawa na tabasamu bashasha kwangu akaniambia achana na wanasiasa hawa maneno matupu hata pesa ya chai hatoi blabla tu.
Mimi nikatowa mshiko pale nijampa akanipa mafundi na gari na vifaa vyote, yule Daniel Yona ilibidi asubiri mimi Pangu Pakavu kazi yangu ifanywe kwanza ndio wamfikirie yeye.
Kwahiyo tangu siku ile nilijufunza kitu kikubwa sana.
Sikushangaa hata kidogo Mkapa na Sumaye kushabikia rushwa na kuita takrima.
Walioiharibu nchi hii kwa kiasi kikubwa ni Mkapa na Sumaye, mnachokiona sasa hivi ni damage control tu.