Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

you are right, watu wengi wanafikiri wazir amekosea but kwa simple evaluation it seem huyu mzee ana mental ilness(psychopathy)
 
huko ni kukosa adabu mbele ya waziri, ikumbukwe kuwa waziri pia ni binaadamu kunawakati hawezi kuvumilia vitu visivyo eleweka
huyo mzee amekosea sana,
 
Kuna kitu tunakisahau kuwa hata hao viongozi wana nyongo pia kama sisi. Japo uongozi ni busara lakini isitumike kama shimo la kutupia takataka kwamba watavumilia tu. Binafsi alivyoanza kujinasibu kuwa ni mtoto wa fulani hapo hapo alikosea.
 
Huyo Lukuvi mwenyewe alikuwa na bonge la scandal la Singasinga, Magufuli akampa maneno yake, halafu akamzawadia wizara nyeti hii.

Hii habari ukiangalia video unaona kwamba wananchi wa Tanzania na viongozi wao wengi sana wana mapepe.
 
hawa takataka watoto wa waasisi huwa wanaamini wao ndio wenye haki kuliko yeyote hapa nchini, hata kujitambulisha hujitambulisha kama wao ndio watoto wa waasisi. wajue kwamba wao ndio wameishaila sana hii nchi kuliko watoto wa wasio waasisi. na waasisi hao hawakuwa mstari wa mbele peke yao, hata wakiongea kuliuwa na wananchi wanawasikiliza na kuwafuata, hivyo wasijione kama wao tu ndio walioisimamisha hii nchi. kwanza ameshafaidi sana nchi hii atoke hapo.

pili, kwa kusikiliza hiyo clip, ni wazi lukuvi alikuwa anajua kabla hiyo issue, na alikuwa anamsikiliza tu. nasema hivi kwasababu inaonekana ni issue ya miaka nenda rudi tangu uhuru huko na imeshapambaniwa sana mahakamani. lukuvi amekuwa waziri hapo kwa miaka mingi na kwasababu ni ndani ya manispaa hiyohiyo ya dsm lazima anaijua hiyo issue, ndio maana kampuuzia kwasababu anajua undani wake.
 
hata ninge kuwa mimi ndio waziri ninge mwambia toka, huwezi kumtishia mtu anaye juwa wajibu wake, na mwendo huu ukiachiwa matokeo yake huzaa majungu, na hatimaye waziri kung'olewa, hapana hii sio sahihi, kweli wanapaswa kuwatumikia wananchi, na pia wanapaswa kuwanyenyekea lkn sio kwa namna hii
 
Pale Iringa alipima viwanja vingi, zaidi ya 12. Sijui anataka vya nini! Anaowatumia watupa taarifa mitaani. halafu anajidai kutatua migogoro Mwanza wakati anafuatilia maeneo ya kupata viwanja!

Mambo ya Lukuvi wanayajua wahehe wenzie! Pale Iringa amemega kiwanja kilichokuwa cha eneo la Mkuu wa mkoa na akajenga nyumba yake!!! Dar amewapimia viwanja wahindi sehemu ya baharini karibu na hotel ya marehemu Ladwa; sehemu ambayo haitakiwi kujengwa OPEN SPACE!!!
 
hiyohiyo ya dsm lazima anaijua hiyo issue, ndio maana kampuuzia kwasababu anajua undani wake.

Usimtete Lukuvi huku huna facts!! Hiyo clip siyo ya Dar ni huko Mwanza Lukuvi anakofukuzia viwanja vyake kabla hajatumbuliwa!!!
 
Inaonekana Lukuvu anaijua hiyo kesi na dhuluma ilivyofanyika. The way anavyomjibu ni kusema hataki kumsikiliza. Lukuvi anaijua hiyo kesi na inawezekana kaambiwa huyo jamaa ndie kakusanya Watu wanaomngoja hapo ukumbini.
 
Huyo jamaa kamfuata Waziri kulalamika kwa sababu huko chini kote kaona hajapata haki.

Kuna tatizo ikiwa nchi mtu hapati haki mpaka aonane na waziri au Rais.
Wasaidizi wa ofisi yake including TISS
 
Ur right kbs ngoja tuishie hapa
 
Inaonekana Lukuvu anaijua hiyo kesi na dhuluma ilivyofanyika. The way anavyomjibu ni kusema hataki kumsikiliza. Lukuvi anaijua hiyo kesi na inawezekana kaambiwa huyo jamaa ndie kakusanya Watu wanaomngoja hapo ukumbini.
Mkuu umeongea kama ninavyowaza mimi, hataki hata kumsikiliza, mbona kuna watu wengi tu wa aina hii na zipo njia za kuweza kumsikiliza mpaka mwisho na ukaelewa? Mara ngapi tunamuona rais anasikiliza watu wa hivi mpaka anaelewa? Naanza kuamini waziri amehusika kwenye hili sababu kama Lowasa alitoa haki kwa hili, ni nani alipata ujasiri wa kutoa umiliki kwa kutengua maamuzi ya waziri aliyepita kwa wizara hiyo hiyo.kwa kutazama tu tokea mwanzo wa clip Kisaikolojia tu unagundua waziri hakuwa anaambiwa kitu ambacho hakijui kwenye shauri hili.
 
hawa watu wa mzanza si ndiowalitaka kumpiga Waitara mpaka polisiw alivyoingilia kati, duh hawa jamaa kwa masuala ya Ardhi ni balaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…