Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 382
Msiba wa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Shambe Sagafu aliyefariki mwanzoni mwa wiki ,uligeuka kuwa uwanja wa siasa baada ya mwenyekiti wa chama hicho Moshi Mjini, Alhaj Omar Amin Shamba kuwashambulia kwa maneno makali baadhi ya makada wa Chama hicho waliojitosa kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi ya ubunge Jimbo la Moshi Mjini mwaka 2020.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya mazishi ya Shambe wakati mwenyekiti huyo akitoa salama za chama nyumbani kwa marehemu eneo la majengo tukio ambalo liliugeuza msiba huo kama uwanja wa siasa huku baadhi ya waombolezaji wakikosoa maneno hayo wakidai hayakuwa pahala pake .
Lakini habari kutoka kwenye msiba huo zinadai kuwa,Mzee Shamba kabla ya kuwashambulia makada hoa alianza kueleza uhusiano wake na marehemu akidai hakuwa na uhusiano naye mzuri na walifikia hatua ya kutokusalimiana lakini akasema miezi mitatu kabla ya kifo cha marehemu wawili hao waliombana msamaha na maisha yakaendelea japo hata hilo halikuwafurahisha waombolezaji.
Inaelezwa baada ya kutamka maneno hayo akawageukia makada hao na kudai baada ya majina yao kukatwa na ngazi za juu za uamuzi za chama baadhi yao walimnunia wakiamini amehusika kuyakata majina hayo na kuhitimisha kwa kuwambia siasa siyo uhasama maneno ambayo yalimwamsha mmoja wa makada waliokuwa sehemu ya watia nia Ibrahim Shayo maarufu kama Ibra Line .
Ibra line kwa upande wake akapiga kijembe na kuwataka baadhi ya wazee kujitathimini na kuchagua maneno na sehemu ya kuyasemea akiamini kuwa mzee Shamba alikosea kutamka maneno yale kwenye mkusanyiko wa watu waliojawa na majonzi kauli ambayo iliwaibua watu wengi na kuanza kushangilia.
Shayo alisema Mzee Shamba hakuwa na sababu yoyote kusema kuhusu msuguano wake na maheremu kwani yalikuwa ni maneno ya kuendelea kuitia simanzi familia yake na ndugu na jamaa walioshiriki tukio la kumstiri ndugu yao.
Pamoja na hayo,Ibra Line kama anavyofahamika na wengi aliipa faraja familia ya marehemu Shambe baada ya kubeba jukumu la kuwasomesha watoto wawili wa marehemu kwenye moja ya shule anazozimiliki.
Kazi iendeleee