15 March 2025
FAMILIA YA Mjumbe wa Kamati ya Siasa (CCM) Mkoani Tanga, Shaibu Juma Mwanyoka Wacharuka
View: https://m.youtube.com/watch?v=BBeNljxHHsU
Walalamika ni wiki moja imepita lakini bado hawajaweza kukutana na kiongozi huyo kigogo kijana wa mkoa wa Tanga ...
Ndugu waongeza, (March 2025) Shaibu Juma Mwanyoka wiki moja iliyopita alikuwepo kwenye msafara wa rais Dr. Samia Hassan alipofanya ziara mkoani Tanga ...
Na kuilalamikia Polisi utaratibu wa ukamataji ulivyofanyika na pia kukosekana haki ya familia na ndugu kupata taarifa au nafasi ya kuonana na mpendwa wao ndugu Shaibu Juma Mwanyoka kada wa CCM aliye mjumbe wa Kamati ya Siasa (CCM) Mkoani Tanga, Tanzania...
Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga ...
Toka maktaba:
Mambo mengi anayofanya mjumbe huyo wa kamati ya siasa ktk kutekeleza shughuli za kichama
19 Agosti 2024
MANYOKA ALILIA UWEPO wa KIWANDA KOROGWE - MBELE ya MAKAMU wa PILI wa RAIS AJILIPUA...
AKIWA KATIKA KAZI ZA KISIASA
MJUMBE wa Kamati ya Siasa (CCM) Mkoani Tanga Shaibu Mwanyoka amesema kwamba,
View: https://m.youtube.com/watch?v=ODeGPg6hYNAShaibu Mwanyoka asema iwapo Wilaya ya Korogwe itapata Kiwanda itaweza kusaidia kuzalisha ajira nyingi kwa vijana huku mama lishe nao wakipata fursa ya kuuza vyakula vyao.
Ndugu Mwanyoka amewasilisha Kilio hicho cha WanaKorogwe mbele ya Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga na Makamu wa Pili wa Rais wa zanzibar Hemed Suleiman Abdullah aliyepo ziarani kwenye Mkoa wa Tanga.
Alisema kwamba, Vijana wengi wilayani Korogwe wamejiajiri kwenye sekta ya Usafirishaji akimaanisha bodaboda ambapo kama kitapatilana Kiwanda wengi wataweza kupata ajira za uhakika na kuongeza kipato chao...