Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga: Tumeshuhudia uchaguzi wa CHADEMA wakitukanana, ni uthibitisho kuwa hawafai kupewa nafasi ya kuongoza nchi

Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga: Tumeshuhudia uchaguzi wa CHADEMA wakitukanana, ni uthibitisho kuwa hawafai kupewa nafasi ya kuongoza nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdulrahman Abdallah, amesema wanasiasa wa vyama vya upinzani hawana cha kuwaeleza wananchi juu ya kile walichokifanya, na kwamba wanafaa kupuuzwa.

Badala yake, amewataka wananchi wamuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

Rajabu ameyasema hayo akiwa wilayani Lushoto, mkoani Tanga, katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, sambamba na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 48 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.

Soma Pia: Tanga: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Amesema kila mtu ameshuhudia jinsi Chadema walivyotukanana na kuvuana nguo kwenye uchaguzi wao, na kwamba huo ni uthibitisho kuwa hawafai kupewa nafasi ya kuongoza nchi.

 
Huyu Mzee ni Mganga wa kutumia MAJINI. Utajiri mkubwa kaupata akiwa Oman na sasa ndiye Mganga wa Kumuagua Mkuu wa Magogoni.
 
Back
Top Bottom