Mwenyekiti CHADEMA, Katavi: Kauli ya James Mbowe dhidi ya Lema inaashiria ukabila, ipingwe na kila mmoja anayependa ustawi wa demokrasia

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela ameeleza kusikitishwa na kauli iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA kutoka jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro James Mbowe dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbless Lema zinazoashiria ukabila

Kujua kauli hiyo, soma James Mbowe: Tabia alizoonesha Lema sio tabia za Wachaga

Akizungumza na wanahabari New Safina Hotel, jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Januari 16.2024 Rhoda Kunchela amesema Godbless Lema ambaye pia amewahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ametumia uhuru na haki yake kutangaza kumuunga mkono Tundu Lissu na John Heche katika kinyang'anyiro cha kutafuta kuongoza chama hicho ngazi ya Kitaifa kwa nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti jambo ambalo limepokelewa tofauti na James Mbowe

Itakumbukwa kuwa baada ya Lema kutangaza kuwaunga mkono Lissu na Heche, James Mbowe alitumia ukurasa wake wa X kuandika hivi, "nimetafakari kwa kina tabia aliyoonyesha ndugu Lema jana siyo tabia za Wachaga"

Akizungumza na Wanahabari Rhoda Kunchela amesema kauli hiyo ya James Mbowe inaashiria ukabila na kwamba ni ya kupingwa na kila mmoja anayependa ustawi wa demokrasia na asiyekubaliana na vitendo vya ukabila nk

Sambamba na hilo Rhoda amemshauri James Mbowe kutoka hadharani na kufuta kauli hiyo na kumuomba msamaha Godbless Lema kwani ikiendelea kubaki inaleta hisia na mapokeo tofauti kwa chama hicho ikizingatiwa kuwa yeye (James Mbowe) ni 'mtoto' wa Mwenyekiti wa sasa anayetetea pia kiti chake Freeman Mbowe
 
Dogo jinga kabisa kazidi kumuharibia babake akidhani anamsaidia.
 
Safi sana
 
Kwahiyo aliitisha press kuongelea hili tu?
 
Back
Top Bottom