TANZIA Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE

Mimi siku nimepata taarifa kupitia channel ya Telegram ya JF ilikuwa saa moja asubuhi nikiwa kwenye Bajaj naelekea kibaruani. Nilishtuka sana, macho yakawa mazito machozi yakaanza kuchungulia japo niliyazuia, sikuamini, huku nikikumbuka jinsi walivyokuwa wanabebisashana na KLyn wake.

Kwa ufupi, wengi sana wameguswa na huu msiba.
 

Mwalimu wangu Mmoja na Bingwa wa Saikolojia aliwahi kuniambia kuwa ukiona Mtu anayatafuta sana Machozi mbele za Watu ili mradi tu nae aonekane analia au Mwingine akiwa anajifanya Kumzungumzia sana Marehemu jua kuwa kama kuna Chuo Kikuu cha Unafiki duniani basi hao ndiyo Wanafunzi Wao waliofaulu vyema na kwa Kutukuka kabisa hilo Somo. Kulia Msibani / Misibani kuna dhana pana sana ipo Siku nitaieleza kwa undani wake na ndiyo maana huwa nikiwa nahudhuria Misiba sehemu mbali mbali huwa nikiwaona Watu wengine ambao nawajua kabisa ' Kindakindaki ' wanaanza Kulia huwa nabaki Kucheka tu Kimoyomoyo.

Kuna Mtu mmoja niliwahi Kuongozana nae katika Msiba mmoja hivi nao ni wa Mtu mkubwa na maarufu hapa Tanzania na cha Kushangaza tukiwa tunajiandaa kwenda Msibani ikiwa ni mida ya Usiku hiyo njia tuliyopita ilikuwa na ' Madada Poa ' wanajipanga ambapo nakumbuka huku akijua tuna Masikitiko na tunaenda Msibani Kwanza alimnunua ' Malaya ' Mmoja na ' Kumbandua ' eneo la Gizani huku Mimi nikiwa nimetangulia kwa mbele kidogo na alipomaliza tu Kupiga ' Kimoko ' chake tukaendelea zetu na Safari na ile Kukaribia tu Geti la Nyumba ya Msiba ghafla alianza Kulia tena pengine hata wale waliofika pale Msibani na Kumtangulia Kulia kiasi kwamba alinipa sana Kazi ya Kuanza Kumbembeleza ndipo akaanza Kupoa na kuwa sawa.

Sasa Kituko zaidi wakati tumeshakaa na kutulia huku harakati na ratiba mbalimbali za Msiba zikiendelea pale nikamuuliza ilikuwaje hadi akalia vile isivyo kawaida ndipo kwa Kinywa chake mwenyewe akanijibu kwamba kama asingelia vile Ndugu wa Marehemu wasingemuelewa na kwamba aliona alie vile ili aonekane yupo nao katika Majonzi makubwa na awemo katika Ratiba ya Ndugu ambao watapanda Ndege pamoja na Mwili wa Marehemu kwenda Mazikoni Kijijini ambako alisema kuwa akienda huko na Msiba ( namaanisha Mazikoni ) baada ya Msiba ana uwezekano na kurudi na Hela nyingi ambayo anaweza hata Kuanzisha Mradi na akajiajiri Kitendo ambacho alikifanya kwani alipojua tu kuwa nae amejumuishwa katika watakaoondoka na Mwili kwa Usafiri wa Mbung'o / Ndege alianza nae Kukusanya Michango ya baadhi ya Waombolozeji waliokuwa pale na hata alipofika huko Mkoani ndiyo alizidisha Juhudi zake za Kukusanya Michango ' Kimagumashi / Kisamjosamjo / Kiujanja ' hali ambayo ilimfanya hadi arudi Dar es Salaam kutoka Msibani awe na Kiasi cha Pesa kama Tsh Milioni Moja na Laki Tano hivi ambayo aliamua Kuiwekeza katika Kuanzisha Biashara ya Kufuga Kuku ndipo Vicheche, Kenge na Mbwa waliokuwa hawachezi mbali na Banda lake alilokuwa ameweka hiyo Mifugo yake nao wakamwambia kuwa hata Wao ' Fursa ' wanazijua vile vile ambapo walimtafunia wale Kuku pamoja na Vifaranga wote ndipo nikaamini kuwa Hela ya Msibani haina masihara na kwamba ina ' Laana ' mbaya mno na inatakiwa Kuheshimiwa sana tu.
 
Nazani kwa mchango wake katika jamii alipaswa atunukiwe nishani ya u-profesor kabisa!!!

Uzi tayari

Naomba mnijuze kuhusu doctorate yake
 
R.I.P DR.REGINALD ABRAHAM MENGI.ILA TUNGEPENDA KUJUA KILICHOMUUA,
MAANA HATUJASIKIA KWAMBA ANAUMWA.
 
So unataka sema aliwahi kukwapua hela sehemu kwa kutumia professional yake?Ndo ukawa mwanzo wa kutajirika?Maana wahasibu tunajuana bana hatuchelewi chengesha mahesabu!
 
Ile inaitwa Honoris causa au udaktari wa heshima kama wa Dr Jakaya Kkikweta
 
Noted....

Jamaa alikua smart coz wahasibu bhana wakipataga fursa huwa wanazitumia vizuri. Sina huhakika kipindi chao Kama walikua na pressure ya GAG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…