Mwenyekiti wa CCM kampa nafasi mwanachama na mjumbe mwenzake kama anatosha kuendelea na kuamua kujihukumu mwenyewe kabla hajahukumiwa

Mwenyekiti wa CCM kampa nafasi mwanachama na mjumbe mwenzake kama anatosha kuendelea na kuamua kujihukumu mwenyewe kabla hajahukumiwa

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Ukiona bosi wako kaamua kukufikishia ujumbe kwa uchungu na tena ikizingatiwa ana moyo wa nyama ni dhahiri anakupa nafasi ya kujipima na kujihukumu mwenyewe. Na mara nyingi njia hii hutumiwa na mkosaji ili kulinda heshima na urafiki wao( Rejea kuondoka kwa waziri mkuu 2008)

Kwa mamlaka yake kamili aliyo nayo, uwezo na nguvu ya kukutoa anao ila anakupa nafasi ya kujichagulia njia rahisi itakayompunzia mkosaji maumivi. Naweza kufananisha na njia za kuchinja mnyama, kuna njia ya kupiga shoti, njia ya kunyong na njia ya kuchinja kabisa.

Kujiuzulu naweza kufananisha na njia ya kupigwa shoti, kutolewa kwa azimio la bunge ni njia ya kunyonga na kuvuliwa kwa kuvuliwa uanachama ni kuchinjwa tena na kitu butu.

Ukiachana na njia hizo mbili ambazo kwa ubunge alionao anaweza kupoteza uspika tu, hiyo njia ya tatu si uspika tu bali hata ubunge atapoteza na kupoteza sifa zote za uanachama ndani ya CCM.

Kujiuzulu ndio njia inayolinda heshima zaidi na kupunguza aibu kwa mkosaji. Ni njia inayopunguza maumivu kwa mkosaji.

Ikitokea hajahamua kujihukumu mwenyewe kwa njia rahisi basi kutakuwa hakuna namna zaidi ya kuhukumiwa.
 
Back
Top Bottom