A
Anonymous
Guest
Katika Mkutano huo pia wadau wengine walikaribishwa ikiwemo viongozi wa dini na viongozi wa CCM, lakini aliyeteka shoo na kutibua hali ya hewa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, huyu mama anaitwa Shemsa Mohamed.
Alielezea mambo mengi ambayo najua viongozi wa Serikali hawakutaka jamii iyajue au kuyasikia ikiwemo masuala ya mauaji uonevu na uvunjwaji wa haki za binadamu unavyoendelea huku mamlaka za usalama ikiwemo Jeshi la Polisi vikiwa kimya na kutaka mambo yasifike kwenye jamii.
Sikiliza sehemu hii ya hotuba ya kiongozi huyo wa CCM alivyoelezea mambo mazito ambayo hata waandishi wa habari waliokuwepo hawakuripoti.
Waandishi wa Habari waliziwa na kupigwa mkwara na watu wa Usalama kuwa 'ole wao watoe hiyo taarifa.'
Natamani ningekuwa mwandishi wa habari nione huyo ambaye anaweza kuzuia habari yenye faida kwa jamii isitoke. Waliowatishia waandishi majina na sura zao niliziona, nawahifadhi kwa sasa, Inakera sana
Baadhi ya mambo ambayo Mwenyekiti huyo wa Chama Mkoa ameyasema ni:
1. Watu wamekuwa wakipotea kwenye mkoani hapo
2. Wizi umezidi, nyumba zinavamiwa usiku na hakuna hatua kutoka kwa vyombo vya usalama
3. Miili ya watu imekuwa wakiokotwa kwenye mifuko ya Rambo
4. Taarifa zinazoandikwa na Jeshi la Polisi sizo ambazo watu wameenda kuripoti
5. Lamadi kuna mtu amepigwa na Polisi akafa kituoni lakini taarifa ikaandikwa tofauti
Kwa ufupi hali ya usalama si nzuri Mkoani Simiyu, RPC wa Simiyu hajatoa tamko wala kuchukua hatua zozote licha ya mambo hayo kuzungumzwa mbele ya hadhara
Jiulize kwa maneno kama hayo ambayo yalitamkwa tarehe 25 mwezi wa tatu mwaka 2023, mamlaka zinakaa kimya kabisa kama vile hakuna kitu kilichozungumzwa cha msingi? Kuna shida mahala