Political Jurist
Senior Member
- Sep 6, 2021
- 143
- 120
MWENYEKITI WA CCM SIMIYU AHAMASISHA WANANCHI KUPIGA KURA.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed, ameendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi leo kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Madeco mjini Maswa Shemsa amesisitiza umuhimu wa uchaguzi huu katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuchagua viongozi waaminifu na wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya wananchi.
Shemsa amewakumbusha wananchi kuwa kupiga kura ni haki yao ya msingi na njia muhimu ya kushiriki katika maamuzi yanayogusa maisha yao ya kila siku.
Pia amewataka wananchi kutanguliza amani na utulivu katika zoezi hilo na kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Wasimamizi za uchaguzi.
Mwenyekiti huyo wa CCM pia amepongeza maandalizi mazuri ya uchaguzi na juhudi zinazofanywa na mamlaka husika kuhakikisha mchakato unakuwa wa haki, uwazi, na usawa kwa wote.