Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan aongoza kikao cha Kamati Kuu, Ikulu

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichokutana Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 26 Septemba, 2022.


Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe Dkt Hussein Mwinyi akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa ccm-Tanzania visawani Mhe Dkt Ally Mohamed Shein muda mchache kabla ya kikao kuanza,



Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Ndg Abdulrahaman KINANA akipitia makabrasha mbalimbali kabla ya kikao cha Kamati kuu Maalum,


Katibu wa NEC Itikadi & Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akiteta jambo na Mjumbe Mpya wa Kamati Kuu Ndg Steven Masato Wassira,


Your browser is not able to display this video.

Wajumbe wa Kamati kuu wakimkaribisha kwa Wimbo wa Chama Mkt wa Kikao Ukumbini,


#CCM MBELE KWA MBELE
 
Kikao Cha ciciem ikulu..
Au Basi.
 
We jamaa anzaga Tanzania na herufi kubwa
 
Safi Sana kwa chama kiongozi , chama kilichobeba matumaini ya watanzania, chama kilichobeba hatima ya Taifa hili, chama kilicho kimbilio la wanyonge, chama kinachotoa dira na muelekeo wa Taifa hili, chama kinachobadilika kulingana na wakati, chama ambacho kimekuwa sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu, chama Cha Hayati baba wa Taifa mwalimu Nyerere,Hakika CCM itaendeleaa kuongoza nchi hii Daima
 
Akili za mashoga hizi.
 
Kiukweli kuna vitu lazima tumsaidie Mama yetu, japo hakuna kosa lolote kikatiba, kisheria, kiutaratibu na kanuni, kuzuia kufanyia vikao cha chama chetu, kwenye ikulu yetu kwasababu CCM ndio chama tawala hivyo ikulu ni yetu, but its morally wrong , hivyo this is crime against morality.

JPM pia alianza hivi hivi, tulipokemea humu akawa msikivu alatusikia akaacha na tukampongeza Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!
P
 
Ikulu siyo ya Ccm, hili ndio kosa kubwa lililopo kwenye mindset za maccm.
 
Endelea kupiga kazi mama we are so proud of you
 
Mhe Mbunge Ikulu ni Ofisi, ya Umma,

Usisahau Kuwa CCM pia ni kipande cha huo Umma,

So, Hakuna shida kabisa
 
We ni mpuliza filimbi wa Watawala, yeyote atakayekalia kiti utaandika vile vile iwe CDM au chama kingine.

Ukihakikishiwa TAKRIMA kdg, maneno yanakutoka, usoni Ukiwa na
TABASAMU la MAMBA!!!!πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
We ni mpuliza filimbi wa Watawala, yeyote atakayekalia kiti utaandika vile vile iwe CDM au chama kingine.

Ukihakikishiwa TAKRIMA kdg, maneno yanakutoka, usoni Ukiwa na
TABASAMU la MAMBA!!!!πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Hivi kwa akili yako unafikiri Kuna chama mbadala wa CCm hapa nchini? Kwa kazi kubwa ya serikali hii ya CCM inayoongozwa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani unazani kuna mwenye ubavu wakuweza kupata kura mbele ya CCM hii? CCM ipo hapa na itaendeleaa kuwepo hapa muda wote maana wananchi wanamatumaini makubwa Sana na chama hiki kilichobeba matumaini ya Watanzania wanyonge
 
Aliyepita alikuwa anafanyiaga wapi

Ova
 
Ila Wewe mwamba nakuelewaga Sana, keep on moving brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…