Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan aongoza kikao cha Kamati Kuu, Ikulu

CCM hata Kama ukiwaona Kwenye kikao ni watu wa tofauti Sana Kwani wamevalia sare vizuri, Wanautulivu wa kutosha simply wako vizuri Sana hawa watu
 
Kinana ndio selemani matola?

Kwanini wanatumia ofisi ya umma kwa vikao vya chama?
Nyinyi kila siku mnasema hii Serikali ya CCM. Ndo maana yake hiyo.
Wakati Mbowe ni kiongozi wa upinzani Bungeni, alipewa gari la Serikali na alikuwa akienda nalo kwenye mikutano yenu.
Hapo Mwenyekiti amewakaribisha wajumbe nyumbani kwake
 
Hivi kwa Sasa mnasimamia Nini kinachogusa maisha ya mtanzania?
CCM imesababisha tupige hatua Kwa kurudi nyuma!!

Tunajenga madarasa na matundu ya vyoo Mashuleni bt mwalimu amepuuzwa.

Anaoahidiwa 23% nyongeza, anaambulia 2.3%. hapo hapo anaundiwa tozo ktk miamala ya kibenki Ili alitoa mshahara wake akatwe hata hiyo nyongeza kdg aliyopata baada ya miaka 6.

Watoto wetu walikuwa wanapata chakula shuleni Serikali ikigharimia, saizi pesa hizo zinanunulia V8.

Tunaitoa CCM madarakani Ili turudi tulipokuwa Ili tuanze hatua vizuri.

Turudishe HAKI Kwa Kila mwananchi afurahie kuitwa MTANZANIA.

Ameeen
 
Nakupenda CCM
 
Miaka michache nyuma hapo ungemuona Humphrey Polepole na Mwalimu wangu Dokta Bashiru Ali Kakurwa na hapo mbele angekuwa Dokta John Magufuli.

Nothing Last Forever....Tuishi
 
Ikulu ni Ofisi ya umma.

Tafuteni pa kufanyika vikao vyenu vya Chama.
 
Mwisho wa agenda muulizane kale ka Utaratibu ka KUJIHOJI na KUJISAHIHISHA aloanzisha mwl Nyerere kaliishia wapi????

Mara hii mmesahau kilichotokea 2020 juu ya sanduku la kura?????

Mnajiandaa na chaguzi zijazo bila KUJISAHIHISHA kujua mlikosea wapi????

Hayupo aonaye kinachoenda Kutokea?????

CCM ni sikio la KUFA, halisikii dawa.

Tusubiri.
 
Naona hiki chama bado kipo kwenye Hangover ya mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu.
Wakati umefika sasa CCM au chama kingine chochote kitakachokuwa madarakani, kitenganishe shughuli zake na shughuli za kiserikali. Hivi vikundi vinaitwa vyama kwa sababu sio mali ya watu wachache waliojiunga kwa hiari yao. Sasa inakuwaje chama kitumie raslimali za wananchi wote kama Ikulu na muda wa watumishi wa serikali kama Rais na Mawaziri? Haya ni matumizi mabaya ya madaraka na ni wizi wa mali ya Umma na uhujumu uchumi. Mikutano kama hii inapaswa kufanyika nje ya saa za kazi au weekend kama watu wanaolipwa na serikali watahudhuria na ifanyike kwenye kumbi za mikutano ya kulipia au kumbi za chama kwa chama kilicho na kumbi zake.
Sio haki walipa kodi/Tozo kugharamia mambo binafsi ya chama kimoja, kama huo upendeleo haunufaishi vyama vingine.
 
Isomeke "Ni mali ya watu wachache"
 
Kwanini wanatumia raslimali zetu wote kama IKULU kuendesha vikao vyao?
 
deal done
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…