Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM umenikosha kwa kumwengua Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba, Dodoma

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Hakika kati ya watu walioenguliwa na CCM katika kugombea Ubunge, mmoja wapo wa wananojulikana sana ni Juma Nkamia wa jimbo la Chemba kule Dodoma.

Huyu Mbunge amekuwa akijipendekeza kinafiki na kwa kuudhi, kwa Rais Magufuli wazi wazi. Amekuwa akitaka muda wa Urais wa Magufuli uongezwe kwa kubadili katiba.
Mapendekezo yake ati muda wa Urais uwe miaka 7 badala ya mitano iliyopo.

Rais Magufuli is on record kusema akimaliza muda wake wa Urais hataongeza hata siku moja, na ataondoka kumpisha mwingine ajaye.

Sasa hizi ngebe za Juma Nkamia sijui alikuwa anafikiria nini, wengine wakisema ati katumwa kupima upepo.

Jibu tumeliona.
Juma Nkamia ni pumba za kisiasa, hakuna aliyemtuma na sasa arudi kwenye kazi yake ya zamani, akatangaze vikao vya kijiji chake.

Kujikomba nako ujinga.
 
Huenda akaibukia kwenye vyeo vya uteuzi kama DED, DAS, RAS, DC au RC.
 
Afadhali maana alikuwa anaichokonoa chokonoa katiba yetu,nadhani atajifunza kuacha kujipendekeza pendekeza ili aonekane
 
Sasa hivi itabidi apakatwe tu hakuna namna
 
Kwa mara ya kwanza JPM kanifurahisha kwa kuyakata majina yafuatayo
1. mwakyembe
2. nkamia
3. chenge

Kwa mtizamo wangu mimi hawa wajinga walijiona kama wao ndio wameibeba ccm pamoja na nchi.
 
 

Attachments

  • VID-20200821-WA0004.mp4
    2.3 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…