LGE2024 Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma aliyekimbia na daftari wakati wa Uchaguzi aripoti Polisi

LGE2024 Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma aliyekimbia na daftari wakati wa Uchaguzi aripoti Polisi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mnakumbuka yule Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Dodoma ambaye siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alikimbia na daftari la wapiga kura akidai kuwa kuna hujuma zimefanyika?

Inaonekana sasa "watu wa system wameanza ku-deal nae.

========================================================

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga leo tarehe 12 Desemba, 2024 ameripoti Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu masuala yaliyojitokeza siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba mwaka huu.

Soma pia: LGE2024 Dodoma: Mwenyekiti CHADEMA akiwasha, apora daftari la wapiga kura baada ya kubaini kuna rafu

Baada ya kuripoti mnamo majira ya saa 4 asubuhi akiwa ameambatana na Mawakili wake, Kiongozi huyo ametumia takribani saa tano ndani ya kituo na baadae kuachiwa kwa dhamana ambapo ametakiwa kuripoti tena hapo siku ya tarehe 17 Desemba, 2024.

Wakizungumza baada ya kutoka nje ya Ofisi za Jeshi hilo wameeleza kuwa hawajaweza kuandika maelezo yoyote hivyo ametumia haki yake kisheria ya kutaka kwenda kutoa maelezo Mahakamani iwapo atakuwa na hatia.

 
Mwana Kondoo ameshinda, Tumfuate
IMG_20241201_103301_304.jpg
 
Wapatikane 100 kila Mkoa Tanzania itasaidia kukua kwa demokrasia Nchini
 
Back
Top Bottom