Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
23aafd9b-fe57-4db0-879d-66277bdd5940.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

c515f14b-326a-4d04-b930-304e98d0e980.jpg

======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
 
Hizi picha wenzake wanazitumia vibaya. Bora akutanenao kimyakimkya tu na matokeo yakiwa mazuri, ndio ajitokeze hadharani kupiga nao picha.

Pia, Mbowe akumbuke kauli za Makamba na kikwete za hivi kariibuni kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.

Kinachofanyika hapa ni sawa na kile ambacho CCM hukifanya kwenye uzinduzi wa miradi mbalimbali ambapo miradi husika hupambwa na watanzania kujazwa matumaini kupitia camera za tv, lakini mwisho wa siku miradi hugubikwa na makandokando tofauti na ahadi za majukwaani.

Utasikia Mama anaupiga Mwingi kwa kuongea tu na Wapinzani(Mbowe).
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

View attachment 2464643

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi .

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Asali

Asali ya nyuki wadogo ina kauchungu kwa mbali, Lakini inafaa kwa kulamba

Mwenyekiti analamba asali

Nasikia bei ya asali haijaathiriwa na Vita vya Ukraine na Russia

Vita inaendelea lakini asali inalambika kama kawaida

Hivi ile vita ya ccm mpya na ccm asili ni nani aliyeamua ushindi, Na iliishia wapi

Tunashauriwa tusitumie vitu vyenye sukari ya kutengeneza lakini inaruhusiwa kutumia sukari ya asili kama asali

Tuendelee kulamba asali kabla mzinga haujabomoka

Mwenyekiti on Fire

Lamba asali mwenyekiti
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

View attachment 2464643

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi .

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Wanayo yaongea yawe yanawekwa peupe.
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

View attachment 2464643

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka, siyo ile ya kupiga risasi watu wakiwa bungeni na kununua binadamu iliyofanywa na Magufuli na akina Polepole na Bashiru. Upinzani siyo uadui.

Hongera Samia kwa kuituliza nchi
 
Hizi picha wenzake wanazitumia vibaya. Bora akutanenao kimyakimkya tu na matokeo yakiwa mazuri, ndio ajitokeze hadharani kupiga nao picha.

Mbowe akumbuke kauli za Makamba na kikwete za hivi kariibuni kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Approach ya mbowe naielewa sana ila kutokana na ulafi wa baadhi ya wenzake ndani ya chama wanahisi kama kuna namna anafaidika na ikulu ya mambuzi.
 
View attachment 2464661

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

View attachment 2464667
======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Mbowe kwisha habari yake, Kinana kamwambia bwashee tulia urambe asali, achana na maboya chalii wangu
 
Back
Top Bottom