Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamis Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
______________________
Update..
Hukumu ya Rufaa ya dhamana ya Freeman Mbowe pamoja Esther Matiko itaanza kusoma majira ya saa saba mchana
Jaji Rumanyika atoa vipengele tisa kumuachoa Mbowe na matikonavyo ni:-
Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika
2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.
3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana
4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana
5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.
6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.
7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani
8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani
9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.
Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.
Tanzania bado Ina majaji kwa hakika. Mola ampe maisha marefu Jaji Sam Rumanyika