Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Bro wewe nii nani unaongea kwa confidence kubwa kiasi hicho!!!!!? . Ujuayo ni ya Leo ya kesho huyajui. Ephraem Kibonde alienda bk kumzika mfanyakazi mwenza, akapews na uemc wa shughuli yote. Tafakari maneno ya Mungu aliyosema. Leo Yuko wapi? Mungu Ni Mambo yote. Step down brother. Muache Mungu afanye yake, hata kwa akina Mbowe anafanya. Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani unavyosikia shetani huwa ubadhani ni lidubwasha fulani la kutisha? Mashetani wapo katika maumbo mengi, huyo ana sifa zote za shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kwa msingi huo wana sababu ya msingi kuomba fidia.
 
Nahisi Mbowe na matiako watakuwa wametia akili kwa sasa. Wamwache aje kupambana na Lissu.

Kibibi cha Lumumba kuna wakati wingu likitanda akili inatoweka kabisa.Nilifikiri ungesoma hukumu ya Jaji msomi Rumanyika ungekaa kimya na kuona aibu jinsi hakimu aliyepandishwa cheo na Rais kuwa Jaji alivyochemsha.

Mosi Hakimu Mashauri alipindisha hukumu ili kukidhi matakwa toka juu.

Pili Hakimu Mashauri hakustahili kupanda daraja la Ujaji kwakuwa daraja la uhakimu lilimshinda.

Tatu mamlaka za kupandisha vyeo zinastahili kutafari upya kama zinaheshimu dhamana walizokabidhiwa na wananchi au wameamua kunajisi madaraka hayo.
 
"Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki"

"Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki"

wale majaji wa Lumumba waje sasa
 
Kuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!

Hii leo atalala fofofo!

Hii leo atawasimlia wakeze!

Hii leo hataisahau kamwe!

Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!

Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!

Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.

Haya sasa jifanye unaumwa tena.

Povu ruksa!
Hata Ephrahim Kibonde alikuwa na kejeri zaidi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi “ - Jaji Rumanyika

“ hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri Lakini Wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi “ - Jaji Rumanyia

“ ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi “ - Jaji Rumanyika

“ Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia HAKI “- Jaji Sam Rumanyika .

Chanzo:Ukurasa wa twitter wa Zitto
Instagram media - ButLKC5h4cR.jpg
 
Uwezekano wa Mbowe kushinda hii kesi ni mdogo kwa kuwa dharau alizofanya zilikuwa za wazi kabisa akitegemea mabwana wake wa Brussels ( EU ) watamtetea, acha apate anacho stahili iwe fundisho kwa wote pia.
Wako huru sasa, your wishes have failed.
 
Hivi unashiriki vipi misa ya kupakwa majivu kanisa moja na wafuasi wa shetani ?
 
Back
Top Bottom