Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Hons Justice RUMANYIKA ukisoma hukumu yake unaona kweli huyu ni jaji wa mahakama kuu,Ni hazina na ameijengea hadhi mahakama
 
Dhamana haki ya yao kilichokuwa kinafanyika sarakasi za maelekezo ya jiwe shetani anakwenda kushindwa leo
Hivi ukiwa chadema lazima tuwe na uwezo mdogo wa kufikirikia ,kama jiwe aliingilia atashindwa nini kuingilia kwa Rumanyika ?mawakili wenu walichemka tu
 
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
========

UPDATE:



Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama Kuu jijini Dar‬


Maneno ya Jaji Rumanyika akisoma hukumu

Mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi. Hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri lakini wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi

Ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi.

Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki.

=====


Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba. Mahakama yaagiza warufani waachiwe mara moja.

Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika

2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.

3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana

4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana

5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.

6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.

7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani

8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani

9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.

Akisoma uamuzi huo leo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri. Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.


Kamwe shetani hawezi shinda ataaibika tu, uchumi tumesha aibika, demokrasia tumeaibika kumuua lisu aibu duniani, saa nane, MO, manji nk aibu kwa serikali ya shetani.
 
umeongea upuuzi, maana hakunaga kitu kama hicho

ebu tupekue vifungu vya sheriw vya kumtetea MBOWE ATOKE NDANI

msaidie mwanasheria kutafuta vifungu na omba atoke

umeongea kama mtanzania halisi na may be std 3 ambaye anauliza maswali badala ya ku focus kwenye KUFANYA jambo litokee
Na wewe umejibu kama Mtanzania halisi ambae baada ya kumsaidia kujibu swali anaporomosha maneno ya kejeli alafu ndo jibu linafuata bila kutambua kwamba katika idadi ya Watanzania sio wote wenye uelewa wa mambo mbalimbali, yeye kauliza swali apate kuelewa
 
Hivi ukiwa chadema lazima tuwe na uwezo mdogo wa kufikirikia ,kama jiwe aliingilia atashindwa nini kuingilia kwa Rumanyika ?mawakili wenu walichemka tu
Mawakili walishindwa nini na leo wameweza nini.
 
Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.

Haya maneno ndio yanayothibitisha kwamba Hakimu Mashauri hakutumia na kuzingatia utashi na weledi wa kazi katika maamuzi yake.
Yeye alitumika kama chombo tu cha hao waliokuwa wanamtumia.


Na kama kawaida yao, watu hawa walitaka kutumia tukio la kuwaweka Mbowe na Matiko Mahabusi kuwa mfano kwa wengine. Waogope na wao yasiwapate kama yalivyowapata Ester na Mbowe na Godbless Lema, na Jualikali, n.k.
Hii ndio njia yao ya kuwatishia watu waTanzania wawaogope na kuwatia hofu.

Jee, waTanzania sasa wamezidi kuwa waoga?

Na Kama waTanzania "si wajinga" kama tulivyoambiwa, watakuwa wamejifunza nini katika tukio hili? Hakuna funzo lolote watakalojifunza?

CHADEMA watafanya nini ili hili funzo liwaingie vizuri waTanzania?

Ni viongozi wa ajabu sana hawa tulionao wakati huu!
 
Yaani spika wetu ni mbaya sana. Kweli kamtesa mama wa watu wakati yeye ndo alomtuma kwa safari jamani. Nimeumia sana kwa kweli.
 
Wewe msukuma nyamaza tutachanga mpaka mafao ya Lissu mshahara tutachanga mpaka kipindi chake cha ubunge kiishe!
 
Akili zinazotumika kutoa ushauri kwa mambo mepesi saa nyingine unakaa na kujiuliza hawa ndio wanadhamana ya kupambana na mabeberu huko duniani je wanawezaje?
 
Wakionekana wanapaswa kuwa nje kwa dhamana, Je watalipwa fidia ya kuwekwa ndani muda wote huo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Thubutuuu...
Kesi hii inadhihirisha kuwa wapo wanasheria waliopo kwa utashi na matakwa ya watu lakini pia wapo waliopo ili kutimiza matakwa ya sheria na kutenda haki.
Majaji na mahakimu wapo kutenda wajibu wa kiMungu katika utoaji haki na adhabu wakikengeuka hilo sijui mwisho wa siku kama Kaizari atawaikoa na adhabu ya milele.
 
Kumbe Matiko alitumwa na Spika Burundi yaani pamoja na kuleta uthibitisho bado alikataliwa? Duuh tuombe uzima kwa kweli ili tuyaone mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunatakiwa sote tuimbe wimbo wa aina moja... neno upinzani halitakiwi kusikika...
Tuna demokrasia yetu ebooo hivi kwanini hatuelewi tunavyoambiwa?
 
Back
Top Bottom