Ila msigombane kama NCCR MAGEUZI pale Tanga kwenye mkutano wao na ndio ikawa mwisho wa zama za chama hicho kutamba kwenye siasa za nchi hii. Mzee Cheyo wa UDP naye aliletewa za kuleta na kina Jidulamabambasi wakiutaka uenyekiti wa chama hicho nacho kikapoteza umaarufu. Njoo TLP ya Mrema na CUF ya Maalim Seif ni yaleyale kama ya wakati huu kwa CHADEMA. Vyama vinakufa kisiasa kwa kutokusikilizana pamoja. Wenzao CCM wanadunda tu na kofia mbili za mwenyekiti wao, yeyote atakayejitokeza anahangaisha chama atashughulikiwa kisawasawa atulie