toka nchi yetu ijikomboe kutoka kwa wakoloni,tumekuwa tukisema tanzania ni nchi yenye amani,utulivu,haki,upendo..mimi hayo maneno sikubaliani nayo hata kidogo.
uko wapi uhuru wa kuzungumza?uko wapi uhuru wa kuhoji?uko wapi uhuru wa kushiriki au kushirikishwa?iko wapi haki?iko wapi democrasia?uko wapi upendo??..KAMA TU
-tukihoji utawala tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishiriki harakati tunakuwa maadui zao
-tukiunga mkono wapinzani tunauzwa kuwa maadui zao
-tukidai haki zetu tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukiandika habari zinazowagusa tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishinda tunanya'ganywa ushindi
-tukishinda uchaguzi unafutwa.
"iko wapi HAKI ndugu zangu?,iko wapi DEMOCRASIA ndugu zangu?"... hivi hii TANZANIA ni ya nani?????????hivi kuna mwenye hati miliki juu ya nchi hii..???
1.ikoo wapi HAKI juu ya kifo cha DR.MVUNGI aliyekuwa kamishna wa tume ya mabadiliko ya katiba baada ya kuvamiwa kwake kimara na kujeruhiwa na watu wasiojulikana na hatimaye mauti yakamkuta akiwa hospitali.
2.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa DK.ULIMBOKA aliyetekwa na kutolewa meno,kupigwa nondo,kukatwa na mapanga kisa tu kutetea haki za madaktari.
3.iko wapi HAKI juu ya umwagiwaji wa tindi kali kwa mwandishi na mtafiti mahiri SAED KUBENEA?
4.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa KAMANDA MAWAZO na hitimaye kukatwa katwa mapinga na baada ya siku moja akafariki...???
IKO WAPI HAKI,UKO WAPI UHURU,IKO WAPI DEMOCRASIA,UKO WAPI UPENDO NDUGU ZANGU????....KIUKWELI INAUMA SANA BWANA,HII NCHI NI YETU SOTE NA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI JUU YA TANZANIA,KWANINI WANATUFANYIA HIVI LAKINIIIIIII???????