Mwenyekiti wa CHADEMA Njombe, Rose Mayemba akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha mgomo wa Wafanyabiashara unaoanzia Kariakoo!

Hoja mfu mkabisa hii. Kwani hakuna watu ambao ni wafanyabiashara na vile vile ni wanasiasa?

Acha uwoga wewe, usiwapangie watu namna ya kuishi. Chawa mkubwa wewe.

Ukisoma vizuri utanielewa nini maana ya nilichoandika, mtazamo wangu ni tofauti kabisa na unachojaribu kuandika.

Tujifunze kuwa na mawazo huru na kukubali hata yale tusiyopenda kuyasikia.
 
Binafsi sitakuwa mzalendo afu wafaidi wengine hivyo sasa nitaendelea kwepa kodi kila dakika inayoenda maana ninapoishi barabara ya lami hakuna
 
Ninachoweza kusema, kama wafanyabiashara wanataka kugoma kushinikiza mambo yanayohusisha biashara zao Vs Serikali wagome bila kushirikisha wanasiasa wa Tanzania.

Wanasiasa nao wakae mbali na movement zinazohusu raia walio nje ya siasa zao ili hizi movement zisiwe na milengo ya kisiasa.
Hao wanasiasa baadhi nao pia ni wafanya biashara huwezi kuwatenganisha mfano Kuna msukuma bungeni Kuna abood Kuna kishimba wako wengi tu asilimia sabini ya wanasiasa ni wafanya biashara ukitaka wasijiusishe basi tutenganishe siasa na biashara
 
Hii ndiyo kazi wanayoiweza Chadema, wao n kupinga tuu

CCM inachoweza ni kutokuwasikiliza wananchi, na kuwalinda viongozi mafisadi, wala rushwa na walaghai. Ndiyo maana huwezi kusikia CCM imechukua hatua dhidi ya mafisadi yanayotajwa kwenye report za CAG kila mwaka, kwa sababu wizi na ufisadi wa viongozi umekuwa ndiyo sera ya chama.
 
Binafsi sitakuwa mzalendo afu wafaidi wengine hivyo sasa nitaendelea kwepa kodi kila dakika inayoenda maana ninapoishi barabara ya lami hakuna

Utawezaje kuwa mzalendo wakati viongozi wote ni mafisadi, wala rushwa na wevi wakubwa? Wengine ndio hao wanaopora rasilimali za Taifa na kuwagawia waarabu. Hata ukitaka kuwa mzalendo, ukalipa kodi vizuri, yanaenda kula hayo mafisadi. Ukiweza, tunza hela yako iwasaidie wanao kuliko kwenda kuibiwa na mafisadi yaliyojaa serikalini.
 
Ninachoweza kusema, kama wafanyabiashara wanataka kugoma kushinikiza mambo yanayohusisha biashara zao Vs Serikali wagome bila kushirikisha wanasiasa wa Tanzania.

Wanasiasa nao
wakae mbali na movement zinazohusu raia walio nje ya siasa zao ili hizi movement zisiwe na milengo ya kisiasa.
Sidhani kama hapo kuna mwanasiasa anahusika,mamlaka ya mapato Tanzania wanafanya rough nyingi sana kwenye sector ya biashara.
 
Binafsi sitakuwa mzalendo afu wafaidi wengine hivyo sasa nitaendelea kwepa kodi kila dakika inayoenda maana ninapoishi barabara ya lami hakuna
Wakati wa Magufuli kodi ilikusanywa kwa jasho na damu na wengi tuliumia lakini at least kulikuwa na tija ya ukusanyaji ule tofauti na sasa kodi inakusanywa inachokifanya hakionekani.

Nasimama na wewe maendeleo hakuna kodi nayo hakuna.
 
Hao wanasiasa baadhi nao pia ni wafanya biashara huwezi kuwatenganisha mfano Kuna msukuma bungeni Kuna abood Kuna kishimba wako wengi tu asilimia sabini ya wanasiasa ni wafanya biashara ukitaka wasijiusishe basi tutenganishe siasa na biashara

Mfanyabishara ni mfanyabiashara na mwanasiasa ni mwanasiasa.

Kishimba, Msukuma nk,wakiwa kwenye siasa wabaki wanasiasa, wakiwa kwenye biashara wabaki wafanyabiashara.

Kipaumbele number moja cha mfanyabiashara huwa ni biashara zake, sasa wanasiasa ambao ni wafanyabiashara wasiende kuleta siasa kwenye movement ambazo ziko kwenye uhalisia wakumsaidia mfanyabiashara na mwananchi.
Msukuma akisimama upande wa wafanyabiashara abaki huku na sio kuwa kigeugeu na kutumikia wale ambao ni wanasiasa wenzake akiwa upande wa siasa ili kunufaisha chama chake.
 
Siasa ni biashara pia ya Kuuza Sera
 
Kuna tetesi Kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba anashikiliwa na Polisi kwa kuhamasisha mgomo wa Wafanyabiashara unaoanzia Kariakoo.

Ikumbukwe asilimia 90 ya Wafanyabiashara wa Kariakoo ni Wakinga kutoka mkoani Njombe

Tutaendelea kufuatilia

Nawatakia Dominica Njema 😃

Kuhusu mgomo soma MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'
Hapo kwenye aslimia 90 ya wafanyabiashara Kariakoo ni wakinga imenifanya nicheke tu.
 
Ninachoweza kusema, kama wafanyabiashara wanataka kugoma kushinikiza mambo yanayohusisha biashara zao Vs Serikali wagome bila kushirikisha wanasiasa wa Tanzania.

Wanasiasa nao wakae mbali na movement zinazohusu raia walio nje ya siasa zao ili hizi movement zisiwe na milengo ya kisiasa.
Yawezekana naye mwenyekiti ni mfanyabiashara.
 
Back
Top Bottom