- Source #1
- View Source #1
WanaJF
Nimekutana na taarifa hii huko mtandaoni. Je, ina ukweli wowote?
Hali ya kiafya ya Mheshimiwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeendelea kuzorota, hali iliyolazimu apelekwe nchini Ubelgiji kwa matibabu ya dharura. Kutokana na changamoto za afya zinazomkabili, madaktari wameshauri apokee matibabu maalum ili kurejesha afya yake haraka.
Wananchi, wanachama wa CHADEMA, na wapenda demokrasia kwa ujumla wanaombwa kuendelea kumuombea, pamoja na kuchangia kwa hali na mali ili kufanikisha matibabu yake. Ushirikiano wa Watanzania utasaidia kuhakikisha Mheshimiwa Lissu anapata huduma stahiki na kurejea katika hali yake ya kawaida haraka iwezekanavyo.

- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na amekuwa mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka huu 2025, hivi karibuni amekuwa na ziara nyumbani kwao Ikungi Singida. Safari hiyo imekuwa ni ya kwanza kuanzia alipopata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama hiko.
Madai
Kumekuwapo na grafiki inayosambaa ikidaiwa ni ya CHADEMA ikileleza kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anaumwa sana na hivyo inatakiwaasafirishwe kwa ajili ya matibabu ya nje ya nchi. Taarifa hiyo pia inawataka wananchi kuchangia michango kupita namba iliyowekwa kwenye grafiki hiyo.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao tumebaini kuwa taarifa hiyo haipo katika vyanzo vya kuaminika vya Chama cha demokrasia na Maendeleo ikiwemo ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa CHADEMA.
Aidha ufuatiliaji umebaini kuwa siku ambayo inaonekana katika grafiki hiyo, Februari 15, 2025 ni siku ambayo Lissu alikuwa mkoani kwao Singida akiwa na afya njema. Ambapo alipokelewa na wananchi mbalimbali wa mkoa huo na baadae kufanya ibada ikiwa ni mara baada ya ushindi aliupata Januari 2025 uliomfanya kuwa mwenyekiti mpya wa Chama hiko.
Ufuatiliaji pia umebaini kuwa namba ya simu iliyowekwa kwa ajili ya michango ni ya mtu binafsi na siyo namba ya chama cha CHADEMA ama ya Lissu mwenyewe hivyo inaonesa pia ni kwa namna gani taarifa hiyo ni ya ulaghai.