Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania wilaya ya Rombo auawa kikatili

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania wilaya ya Rombo auawa kikatili

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Inasikitisha sana mauaji kama haya kufanyika kwa mwalimu anayefundisha taifa la kesho.

---
Mwalimu.png

Picha: Mwalimu Turo Hiza enzi za uhai wake
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Rombo na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Boma iliyopo Tarafa ya Mkuu Wilayani humo, Turo Hiza amekutwa ameuawa na kisha mwili wake kutelekezwa barabarani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ,Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Hamis Maiga amesema mwili wa Mwalimu huyo umekutwa usiku wa kuamkia leo ,Mei 26, 2022 eneo la Mrere Mashati karibu na Shule ya Sekondari Shauritanga iliyopo wilayani humo.

"Tukio hili limetokea leo majira ya saa 10 alfajiri eneo la Mrere Mashati,karibu na shule ya Sekondari Shauritanga ambapo mwili wa mwalimu Hiza umekutwa barabarani huku damu zikiwa zinachuruzika kwenye lami,” amesema Maiga.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba mwili wake umekutwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Hata hivyo baada ya mwalimu huyo kuuawa wauaji hao waliondoka na pikipiki yake ambayo alikuwa akiitumia kama usafiri wa kwenda kazini.

Mwili wa mwalimu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma wilayani humo.

Chanzo: Mwananchi
 
Pole kwa familia. Polisi waje na matokeo yanayoeleweka ya uchunguzi. Polisi wakaionyeshe dunia kuwa Tanzania ina wabobezi wa uchunguzi.

Wananchi nao watoe ushirikiano wa kutosha. Hasa kuhusu background ya huyo mwalimu.
 
So Sad kwa mwalimu akiwahi kazini kwenda kufundisha watoto wetu lkn ndio hivyo tena hatunae.
Mungu ampumzishe mahala salama.
Aaaaaamin
 
So Sad kwa mwalimu akiwahi kazini kwenda kufundisha watoto wetu.
Huenda alikuwa ndie mwalimu wa zamu lkn ndio hivyo tena hatunae.
Mungu ampumzishe mahala salama.
Aaaaaamin
Mwalimu mkuu huwa hashiki zamu, pia huwa hawafundishi sikuizi. Japo kawaida inatakiwa awe na vipindi vya kufundisha.
 
1653562218987.png

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Rombo na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Boma iliyopo Tarafa ya Mkuu Wilayani humo, Turo Hiza amekutwa ameuawa na kisha mwili wake kutelekezwa barabarani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Hamis Maiga amesema mwili wa Mwalimu huyo umekutwa usiku wa kuamkia leo ,Mei 26, 2022 eneo la Mrere Mashati karibu na Shule ya Sekondari Shauritanga iliyopo wilayani humo.

"Tukio hili limetokea leo majira ya saa 10 alfajiri eneo la Mrere Mashati, karibu na shule ya Sekondari Shauritanga ambapo mwili wa mwalimu Hiza umekutwa barabarani huku damu zikiwa zinachuruzika kwenye lami,” amesema Maiga.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba mwili wake umekutwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Hata hivyo baada ya mwalimu huyo kuuawa wauaji hao waliondoka na pikipiki yake ambayo alikuwa akiitumia kama usafiri wa kwenda kazini.

Mwili wa mwalimu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma wilayani humo.

Chanzo: Mwananchi
 
Aisee mrere,mitaa yangu hiyo,pole sana kwa familia yake
 
Mwalimu mkuu huwa hashiki zamu, pia huwa hawafundishi sikuizi. Japo kawaida inatakiwa awe na vipindi vya kufundisha.
Hapana siyo kweli kwamba Mwalimu Mkuu/Mkuu wa Shule kwamba hawafundishi, wanafundisha sana sema kinachotokea ni kwamba wanakuwa na vipindi vichache kutokana na majukumu mengi waliyonayo.
Note : Kuna baadhi ya Walimu wakuu/ Wakuu wa Shule wana vipindi vingi zaidi ya Walimu wa kawaida.
 
So Sad kwa mwalimu akiwahi kazini kwenda kufundisha watoto wetu.
Huenda alikuwa ndie mwalimu wa zamu lkn ndio hivyo tena hatunae.
Mungu ampumzishe mahala salama.
Aaaaaamin
Haina tofauti na kumpiga manati na kumuua ndege mwenye vifaranga ambavyo bado havijafungua macho tunduni.
 
Back
Top Bottom