LGE2024 Mwenyekiti wa Kitongoji alieshinda (Chadema) atimuliwa kwenye kikao cha WDC Iramba, Singida

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kiomboi ni mji mdogo bro,hakuna halmashauri za vijiji.
 
Mpuz kweli huyo

Subiri waje wakane

Ova
 
Diwani ni mwenyekit wa WDC na mwenyekiti wa kitongoji sio mjumbe WDC Mwenyekiti wa kijiji ndio mjumbe halali. Diwani yupo sahihi kulingana sheria za TAMISEMI
Ungeinukuu hiyo Sheria ungekua umefanya jambo la Muhimu sana Kwa faida ya wengi!
Kwakua hujanukuu tunashindwa kukutofautisha na Diwani!
Kwakua hukuona umuhimu wa kuinukuu au uliona ukapuuza tu tunakufananisha na CCM wa sasa ambao kwao kufuata utaratibu waliojiwekea wenyewe wanaona changamoto na shida!
Jitofautishe na wao itakujengea credibility!
Tuwasilishie Sheria na kanuni zake kama zilivyotungwa na waziri wa tamisemi!
 
Mwenyekiti wa kitongoji alifata nini WDC wakati yeye sio mjumbe?
 
Yani kinachoenda kutokea ni sawa na rwanda wahutu na watutsi ila tanzania ni ccm na chadema. Itafika muda kupata huduma uwe na kadi ya ccm.
Hivi hawa watu wana shida gani?
Kwa kifupi hatukustaarabika kupokea na kujiunga na mfumo wa vyama vingi. Ndio maana yote hayo yanayokea.
 
Wakati nafanya kazi Halmashauri wenyeviti wa vitongoji hawakuwa wajumbe wa WDC.Inawezekana siku hizi ni wajumbe
 
Diwani ni mwenyekit wa WDC na mwenyekiti wa kitongoji sio mjumbe WDC Mwenyekiti wa kijiji ndio mjumbe halali. Diwani yupo sahihi kulingana sheria za TAMISEMI
Kabisa,kitingoji sio mjumbe wa WDC bali ni mjumbe wa H/ Kijiji husika,diwani yupo sahihi kumtimua
 
Wa vitongiji ni wajumbe wa wdc

Naomba kujuzwa
 
Sheria ipi mwenyekiti wa kitongoji anaingia wdc ?
 
Sio mjumbe kivipi?Nimeandika huko juu kuwa, Kiomboi ni mji mdogo,ila Bado wanatumia vitongoji badala ya mitaa.
Amechaguliwa kama mwenyekiti wa kitongoji haruhusiwi kuingia kwenye wdc. Itakuwa alikuwa mgeni mwalikwa tu. Lakini si mjumbe halali wa wdc
 
Ccm mbele kwa mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…