KERO Mwenyekiti wa Mtaa Mabibo Sahara anatusumbua kwa michango yake ya Ulinzi Shirikishi

KERO Mwenyekiti wa Mtaa Mabibo Sahara anatusumbua kwa michango yake ya Ulinzi Shirikishi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Mabibo Sahara, kero yangu/yetu wakazi wa huku tunachangishwa pesa za ulinzi shirikishi kwa maelekezo ya mwenyekiti, shida siyo kuchangishwa fedha kwa ajili ya ulinzi shirikishi kama mtaa, je ni sawa kuchangishwa kila chumba kwa nyumba moja yaani sio nyumba ila kila chumba shilingi elf 3.

Je ni sawa kwani fedha ya ulinzi inalipwa kwa nyumba au kila mpangaji anaeishi kwenye nyumba husika maana sio kwamba wapangaji tunachanga kwa ajili ya nyumba husika hapana ila watu wa mwenyekiti wanagonga mlango kila chumba kwa kila nyumba kudai shilingi elf 3 ya ulinzi na fedha kwa ajili ya usafi wa mazingira pia ni hivyo hivyo je ni sawa na kama ni sawa mbona kwingineko sio hivyo au tupo nchi tofauti?

Wanatumia fursa hiyo kwa sababu mtaa huu wanaishi wanafunzi wengi wa vyuo kwahiyo nyumba nyingi zimetengenezwa kwa mfumo wa upangishaji na wenye nyumba hizo wengi wao hawaishi pamoja na wapangaji
 
Vikao vya serikali ya mtaa Huwa mnakaa na kufikia muafaka huo,
Kwanini hayo maswali usiulize kwenye vikao vya serikali ya mtaa ambavyo mwenyekiti wa kikao ni mwenyekiti wa mtaa.
 
Back
Top Bottom