LGE2024 Mwenyekiti wa Mtaa wa Malindi Estate, Mbweni, Celina Mkonye (CPA)aahidi kusimamia mikopo kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu

LGE2024 Mwenyekiti wa Mtaa wa Malindi Estate, Mbweni, Celina Mkonye (CPA)aahidi kusimamia mikopo kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Don Gorgon

Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
35
Reaction score
68
Bwashee, mtaa wako una Mwenyekiti mwenye Kiti na CPA? 😀 Basi kutana na Celina Mkonye wa kule Mbweni.

Mara baada ya kula kiapo cha utii na uadilifu, Mwenyekiti aliyechaguliwa wa Mtaa wa Malindi Estate, CPA Celina Mkonye amewaahidi wananchi katika mtaa huo kusimamia mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Ahadi zingine alizotoa CPA Celina kwa wananchi wa mtaa wake ni pamoja na kusimamia utawala bora kupitia wajumbe wake na yeye mwenyewe, ulinzi na usalama, ustawi wa jamii, kuboresha miundombinu pamoja na mazingira.

Wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa 106 na wajumbe 530 kutoka katika kata 20 za Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wameapishwa leo Novemba 28, 2024 katika Ukumbi wa Soko Kuu la Magomeni kuanza kazi rasmi. Wamekula kiapo mbele ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Hanifa Hamza.

 
Back
Top Bottom