Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Stop Over kwa Kapinga ni mwizi wa pesa za ulinzi shirikishi

Unajua nchi hii Askari polisi Ni wachache kulingana na mahitaji na population ya watu, Askari mmoja anahudumia watu Laki 3 kwa idadi ya waliopo, kitu ambacho hakiwezekani.

Ikaonekana wanahitaji msaada kuhudumia wananchi, ndio likaja wazo la polisi jamii, Achana na Mgambo hapo, Unakuta kata Ina migambo 20 na mitaa zaidi ya 7 na mitaa vitongoji 30 Sasa hao mgambo wanasaidia nini?

Mtaani kwangu nilishauri Kama watu hawataki kuchangia Ulinzi Shirikishi Basi angalau kila nyumba aamke mtu alinde kwa zamu, wakiamka 20 Leo na kesho, siku zinazo wataamka wengine, hatuwezi tuchangie vijana wafanye kazi.
 
Askari polisi sio wachache sema wameharibu uaminifu kati yao na raia ndio maana usiku wanakimbia kulinda. Shida hapa sio kulipa hiyo pesa tatizo lipo unalipa pesa halafu hakuna hata mlinzi mmoja. Polisi wapo wachache kulinda raia ila wapo wengi kulinda mikutano ya CCM.
 
Simple, Itisheni kikao na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Mkuu wa kituo Cha polisi jilani, OCD pia awepo mjadili namna gani zoezi liendeshwe,

Kwa malipo sehemu zenye mkusanyiko wa nyumba nyingi Mara nyingi ni 2000_3000 na eneo dogo Ni 5000.

Pia niweke namna Bora ya malipo, Mlisema kuwe na akaunti maalumu kila mwezi mchangie mtashindwa, maana sio wote wanapenda kuchangia hiyo pesa. Ivyo hao vijana wateue watu kadhaa washirikiane na mabalozi wa nyumba kumi kupiga kila nyumba kukusanya na kutoa risiti, hizi za kawaida.

Mapto na matumizi yawe recorded kwa ajili ya mrejesho katika vikao vya mbeleni.
 
Wewe unalala usiku unajamba tu utawaonaje? Nyie ndio Mpaka mkiibiwa hizo flat screen zenu mnaanza kueanyooshea kidole vijana wa watu. Binafsi mtaani kwangu nachangia Ulinzi na nikiwakuta usiku nawatoa hata ya kahawa
Hahaa huwa silala kihivyo mkuu Nina ofisi yangu hapohapo home kwangu nimeweka na mlinzi binafsi, ila Hawa sungusungu sijawahi kuwaona ila wakusananya fedha za ulinzi wanapitaga kwangu mwanzoni mwa mwezi sijawahi kuwapa hela
 
Huyu kwetu mjumbe na mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni wezi hasa ulinzi hakuna huyu mjumbe kutwa kuchangisha 10,000.
Mtaani kwetu ulinzi wala hakuna ila wanajifanya wanaopita kukusanya fedha hata maeneo ambayo kuna walinzi
Tatizo sijui hawajielewi au ndio kutaka kuwaibia watu.
Kuna siku jamaa waliibiwa halafu huwa wanachangia hizo fedha za sungusungu so wakaenda odisini kwa Mtendaji wa Mtaa kudai fidia wakatoswa .
Yaani unalipa hela ya sungusungu then unaibiwa halafu hao sungusungu hata hawawajibiki unaambiwa karipoti polisi
 
Kwanza hakunaga mjumbe wa kata. Pili, m/kiti wa s/mtaa hana mamlaka ya kukusanya fedha ya aina yeyote ile kwenye mtaa, yeye ni mwakilishi wa wanchi tu pamoja na wajumbe wake, mwenye majukumu ya kiutendaji na uratibu wa shughuli yeyote ile katika ngazi ya mtaa ni Afisa Mtendaji ngazi ya mtaa... Mkiti ni mwakilishi wa wananchi na anatakiwa ampe ushirikiano tu Afisa Mtendaji, hivyo kama Mkiti wenu anafanya hivyo anakosea sio jikumu lake ni tamaa tu zinampeleka. Nimeeleza ili ufahamu maana umeandika vitu havieleweki.
Pia swala sungusungu ama polisi jamii hilo zoezi linafanyika kupitia nguvu za wananchi kwa utaratibu utakao wekwa na ofisi ya s/mtaa na Afisa Mtendaji kama mratibu ili pesa zinazo kusanywa walengwa walipwe.. Hivyo ni tofauti na taka ni tenda inayo tangazwa na halmashauri moja kwa moja.. Ili MTU upate lazima uwe na kampuni iliyo sajiliwa na utaratibu fedha pia tofauti na ndio maana kuna pos an efd machine kwa sababu hizo kampuni nazo lazima zilipe kodi
 
We jamaa ni Mtendaji hakii[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Fedha zote za mtaa zinatakiwa zikusanywe kwa kutumia POS machine na risiti ya EFD itolewe kwa kila pesa inayokusanywa na mtaa husika. Hata kama no ulinzi shirikishi fedha hizo hukusanywa na na kuwa deposited kwenye akaunti ya mtaa kabla ya kutumia.
Akaunti ya Mtaa unajua inavyoendeshwa?
 
Nilihamia mtaa mmoja nikakuta huu utaratibu...nikalipia kama miezi minne. Nikaibiwa home....nikawasubiria waje kukusanya hiyo pesa.

Walipofika nikawaambia kwanzia leo sitotoa hiyo pesa. Yaani niibiwe mali ya malaki halafu bado niwalipe watu ambao hata sijaingia nao mkataba wa ulinzi?
Toka siku hiyo mpaka leo hao jamaa hawajaona tena hela yangu. Hiyo ni huduma ya hiari na hailazimishwi. Hakuna sheria inayomtaka raia wa nchi hii alipie hela ya ulinzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…