Salaam ndugu zangu,
Kuna hii habari nimekutana nayo kwenye mitandao ya kijamii ikieleza Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amebeti pesa za simba.
Je, ina ukweli?
Kuna hii habari nimekutana nayo kwenye mitandao ya kijamii ikieleza Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amebeti pesa za simba.
Je, ina ukweli?
- Tunachokijua
- Murtaza Mangungu ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Simba Sports Club ya Tanzania. Leo Januari 21, 2024 Klabu ya Simba ilikuwa katika Mkutano wake Mkuu uliohudhuriwa na Wanachama mbalimbali.
Katika Mkutano huu Murtaza Mangungu na viongozi wengine walipata muda wa kuzungumza mbele ya Wanachama wa Simba SC. Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa ni pamoja na suala la mapato na matumizi ambayo pia halikuwa yanatolewa na vyombo mbalimbali nchini.
Kutokana na hali hii, kumeibuka uvumi kupitia ukurasa uliojinasibu kuwa ni wa East Afrika TV ukimhusisha Murtaza Mangungu. Taarifa hiyo ilibainisha kwamba Mwenyekiti wa Simba alisema kuwa pesa ambazo timu Simba ilizivuna katika kombe la Mapinduzi Cup (Milioni 70) zimeisha kwa wamezitumia kubashiri katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Morocco.
Kuna ukweli kuhusu uvumi huu?
JamiiCheck imepokea uvumi huu na kupitia katika kurasa zote za East Africa Television ili kuhakiki lakini taarifa hiyo iliyoletwa na mleta mada haikuwapo.
Pia, JamiiCheck imechunguza na kubaini aina ya maandishi (Font) iliyotumika katika grafiki hiyo inayosambaa (Blooming Elegant) haifanani na ile inayotumiwa na kurasa za East Afrika TV (Tafel Sans SC Bold It) katika grafiki zao wanazotolea habari nyingine.
Aidha, East Afrika TV wametoa taarifa maalumu kukanusha uvumi huo uliosambaa siku ya Januari 21, 2024. Katika habari hiyo wameeleza:
FAKENEWS: Habari hii sio ya kweli, #EastAfricaTV hatuhusiki na habari hii.
Habari iliwekwa na EATV kukanusha uvumi wa kauli iliyosambazwa
HIvyo, kutokana na hoja hizi JamiiCheck imejiridhisha kwamba taarifa hii iliyosambazwa haina ukweli.