GE2025 Mwenyekiti wa TANECU, Karimu Chipola amuombea kura Mgombea Urais CCM Rais Samia

GE2025 Mwenyekiti wa TANECU, Karimu Chipola amuombea kura Mgombea Urais CCM Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Tandahimba na Newala (TANECU LTD) Karimu Chipola amemuombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo, hususan zao la korosho

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya ubunge wa Jimbo la Newala Vijijini, Chipola aliwaeleza wananchi na wakulima kuwa Rais Dkt. Samia ameonesha dhamira ya kweli ya kuinua kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za ruzuku kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo bure

Akiwa kiongozi wa TANECU, Chipola ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania imefanikiwa kuzalisha korosho kwa wingi mkubwa hadi kufikia tani 528. Aidha, korosho hizo zimeuzwa kwa bei ya juu ya kihistoria ya shilingi 4,195 kwa kilo kupitia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX), hatua ambayo imeongeza uwazi na ushindani katika biashara hiyo


 
Back
Top Bottom