Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika hali inayoonekana kulewa madaraka na utovu wa nidhamu nchini, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kheri James ametoa maneno yasiyo na staha kwa viongozi wetu wa kiroho nchini kwa kuwaambia kuwa washike adabu zao.
Hii inafuatia baada ya viongozi hao akiwemo Sheikh Ponda, Baba Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki na Baba Askofu Bagonza, Baba Askofu Mwamakula, Sheikh Katimba na wengineo kutaka Uchaguzi utendeke kwa haki na kwamba tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC itende haki katika Uchaguzi kwa kutoengua wagombea wa upinzani bila sababu za msingi.
Kijana huyo aneyeonekana amevimbiwa madaraka ambapo mara kadhaa amekua akitoa kauli za kuashiria vurugu, kuchochea vurugu nchini hasa pale alipokuwa akihimiza wanachama wa UVCCM kuwa tayari kuwapiga wapinzani.
Majuzi Dr Bashiru alitoa kauli kuwataka vijana wa UVCCM kujibu hoja za wapinzani lakini badala ya kujibu hoja za wapinzani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM anashambulia na kutukana Mababa Askofu na Masheikh nchini.
Hii inaonyesha ni kwa namna gani Chama Cha Mapinduzi kwa sasa chini ya Mwenyekiti wake ndugu Magufuli na Katibu wake Mkuu ndugu Bashiru Ally kimeshindwa kuthibiti nidhamu ndani ya Chama hicho.
Kimekuwa ni Chama kisichopenda kuambiwa ukweli, bali kusifiwa na kupewa maneno ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa
Hapa chini hii ni video ikimuonyesha kijana huyo akitukana na kufokea viongozi wetu wa dini.