Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM atukana viongozi wa dini nchini, asema washike adabu zao!

Status
Not open for further replies.
Huyu heri bila shaka akili yake ni kibaba. Hakuna siku anapoongea jbo la maana.

Huyu naambiwa ni ndugu yake Mwenyekiti. Labda amerithi baadhi ya genes za tabia ya mjomba maana naye kwa kuropoka, hajambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)

CCM imetufikisha hapa.
Wakisoma watanuna sana.Hivi siyo tupo katikati ya uchumi(mchumiko wa kati)😂😂😂😂😂😂😂
 
Hivi UVCCM wana maslahi gani na engua engua? Hebu tazama!
Aliye engua wagombea ni tume.
Walioenguliwa ni wapinzani
Wanaokemea engua engua ni viongozi wa kiroho
Wanaolalamikiwa kwa engua engua ni tume!
Wanaochachamaa kupinga kemea ya viongozi wa kiroho kuhusu engua enguani ni UVCCM!!
Tume wako kimya, wameyasikia ya viongozi wa kiroho, na huenda wagombea wanaorejeshwa ni kwa kuitikia wito wa viongozi hao wa kiroho.
Hivi UVCCM mbona mnajifanya kurugenzi ya tume ya uchaguzi?
Katibu Mkuu wa CCM amewatuma kujibu hoja za wapinzani, kwa maana ya CUF, NCCR, ACT, CHADEMA, TLP n.k.
K.K.K.T, AGAPE, R.C, BAKWATA, HINDU n.k. si sehemu ya wapinzani. Hujawahi kusikia wanashambulia CCM. Wao wako busy na kunyoosha mfumo wa utawala kwa kujibu wa katiba ya Tanzania, wala hawajui katiba ya CCM inasemaje, haiwahusu.
Hii tume ya uchaguzi ni tume ya Taifa siyo ya CCM, Iache ijijibie tuhuma zao, CCM kujibu tuhuma za Tume ni kijivika koti lisilolako.
 
Duuu haki ya nani, kweli tuna kazi kulea vijana kama hawa.
 
Katika hali inayoonekana kulewa madaraka na utovu wa nidhamu nchini, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kheri James ametoa maneno yasiyo na staha kwa viongozi wetu wa kiroho nchini kwa kuwaambia kuwa washike adabu zao.

Hii inafuatia baada ya viongozi hao akiwemo Sheikh Ponda, Baba Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki na Baba Askofu Bagonza, Baba Askofu Mwamakula, Sheikh Katimba na wengineo kutaka Uchaguzi utendeke kwa haki na kwamba tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC itende haki katika Uchaguzi kwa kutoengua wagombea wa upinzani bila sababu za msingi.

Kijana huyo aneyeonekana amevimbiwa madaraka ambapo mara kadhaa amekua akitoa kauli za kuashiria vurugu, kuchochea vurugu nchini hasa pale alipokuwa akihimiza wanachama wa UVCCM kuwa tayari kuwapiga wapinzani.

Majuzi Dr Bashiru alitoa kauli kuwataka vijana wa UVCCM kujibu hoja za wapinzani lakini badala ya kujibu hoja za wapinzani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM anashambulia na kutukana Mababa Askofu na Masheikh nchini.

Hii inaonyesha ni kwa namna gani Chama Cha Mapinduzi kwa sasa chini ya Mwenyekiti wake ndugu Magufuli na Katibu wake Mkuu ndugu Bashiru Ally kimeshindwa kuthibiti nidhamu ndani ya Chama hicho.

Kimekuwa ni Chama kisichopenda kuambiwa ukweli, bali kusifiwa na kupewa maneno ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa

Hapa chini hii ni video ikimuonyesha kijana huyo akitukana na kufokea viongozi wetu wa dini.

May go to hell
 
Hivi ameoa au kuolewa huyu jamaa au ni Pole Pole, Patambi, Kunambi Type
 
Huyu kijana ni mpuuzi na hana adabu kabisa ... Huu ujinga haukuwepo siku za nyuma mpaka awamu hii ilipoanza. Ubabe wa bwana mkubwa unawapa kiburi subordinates wake.

Awamu hii imethibitisha kuwa katiba mpya inahitajika sana .... DC wa awmu hii utafikiri ni wa enzi za Mkoloni!!
 
Na hili ndo tatizo la kugawa vyeo kwa undugu bila merit, anajua hakuna wa kumgusa kwa sababu kashikwa mkono akae pale
 
Katika hali inayoonekana kulewa madaraka na utovu wa nidhamu nchini, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kheri James ametoa maneno yasiyo na staha kwa viongozi wetu wa kiroho nchini kwa kuwaambia kuwa washike adabu zao.

Hii inafuatia baada ya viongozi hao akiwemo Sheikh Ponda, Baba Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki na Baba Askofu Bagonza, Baba Askofu Mwamakula, Sheikh Katimba na wengineo kutaka Uchaguzi utendeke kwa haki na kwamba tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC itende haki katika Uchaguzi kwa kutoengua wagombea wa upinzani bila sababu za msingi.

Kijana huyo aneyeonekana amevimbiwa madaraka ambapo mara kadhaa amekua akitoa kauli za kuashiria vurugu, kuchochea vurugu nchini hasa pale alipokuwa akihimiza wanachama wa UVCCM kuwa tayari kuwapiga wapinzani.

Majuzi Dr Bashiru alitoa kauli kuwataka vijana wa UVCCM kujibu hoja za wapinzani lakini badala ya kujibu hoja za wapinzani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM anashambulia na kutukana Mababa Askofu na Masheikh nchini.

Hii inaonyesha ni kwa namna gani Chama Cha Mapinduzi kwa sasa chini ya Mwenyekiti wake ndugu Magufuli na Katibu wake Mkuu ndugu Bashiru Ally kimeshindwa kuthibiti nidhamu ndani ya Chama hicho.

Kimekuwa ni Chama kisichopenda kuambiwa ukweli, bali kusifiwa na kupewa maneno ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa

Hapa chini hii ni video ikimuonyesha kijana huyo akitukana na kufokea viongozi wetu wa dini.

Chama cha wahuni
 
Hofu ya kushindwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom