PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Dodoma: Baadhi ya wabunge wanachukulia poa mamlaka ya Rais

PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Dodoma: Baadhi ya wabunge wanachukulia poa mamlaka ya Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba amesema wapo baadhi ya wabunge wamezidiwa na vyeo vyao na kuchukulia poa’ mamlaka ya Rais, hivyo amebainisha kuwa jumuiya hiyo haitokubali kuona wabunge hao wakitweza madaraka ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwanyemba ametoa kauli hiyo Ijumaa Mei 30, 2025 Jijini Dodoma katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa muda mchache kabla ya kuzinduliwa kwa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Bila kukupepesa macho, bila woga wowote, kuna baadhi ya wabunge kama wamezidi na vyeo vyao, kama wanachukulia poa mamlaka ya Rais, wasichukulie poa mamlaka ya Rais, sisi tuko hapa kwaajili ya kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan na kukilinda Chama cha Mapinduzi na mali zake,” amesema.

 
Back
Top Bottom