PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Kagera: Msitupangie cha kuzungumza kuhusu Rais Samia

PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Kagera: Msitupangie cha kuzungumza kuhusu Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera ndugu Faris Buruhani ametoa wito kwa vijana kuendelea kuyasema mema na mazuri yanayofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan bila uoga kwani kazi aliyoifanya kwenye nchi yetu kwa miaka minne ni ya mfano na hakuna sababu ya kukataa kusema au kupangiwa cha kusema kuhusu Rais wetu.

Akiwa na mwaka mmoja tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alileta Milioni 700 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Chuo cha Afya Kagemu kilichokuwa kimechakaa kwa sababu ya ukongwe wake kwani zaidi ya miaka 20 kilikuwa hakijafanyiwa marekebisho yoyote.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kampeni maalumu ya kutafuta kura mpya za Mama Samia ijulikanayo kama SAMIA NEW VOTERS CAMPAIGN [SANEVO] inayoendeshwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM mkoa inaendelea mkoani Kagera kwa kuendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya vijana.

 
Mpumbavu huyo anatafuta kusikika ili apate teuzi. Yeye na uvccm wenzake wote ni mbumbumbu. Rais ana wasemaji wake, angekua na akili hata kidogo angesema mwenyekiti Samia maana ni mwenyekiti wake.
 
Back
Top Bottom