Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohammedi Kawaida .Kwa uchungu,maumivu,simanzi ,majonzi na huzuni isiyopimika wala kuelezeka.
Ameshiriki na kuhusika katika shughuli zote za kuaga na kuupumzisha Mwili wa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Machinjioni Makongorosi wilayani Chunya Mkoani Mbeya, Marehemu Michael Kalinga katika Nyumba yake ya Milele.alipoteza Maisha kutokana na kuuwawa kikatili na baadaye Mwili wake kutelekezwa.
Ambapo Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ameweza kubeba Mabegani pake Jeneza Lenye Mwili wa Marehemu Michael Kalinga ambaye kwa sasa Ametangulia Mbele za Haki.
Kwa hakika kifo kinaumiza sana na wala hakizoeleki hata kidogo,hasa pale ambapo kifo hicho kimetokana na kukatishwa uhai na watu wenye roho za kishetani na waliojaa ushetani ndani yao. Kwa hakika Watanzania wote hatuna budi kukemea vikali sana matukio ya namna hii bila kujali itikadi zetu za kisiasa.. Ni lazima tukatae kabisa kumwagilia ardhi yetu kwa Damu zisizo na hatia.
Kwa sababu Damu ya mtu inazungumza hata kama mdomo na kinywa chake kimefumba.Kwa hiyo Damu zisizo na Hatia zikianza kuzungumza na kulia kwa wingi kutoka Mavumbini zilipomwagwa kuelekeza kilio chake machoni, usoni na masikioni pa Mwenyezi Mungu .Basi inaweza kuleta dhahama kutoka kwa Mungu Mwenyewe pale atakapoamua kusikiliza Madai na kilio cha Damu hizo zilizomwagwa Bila Hatia.
Vilio hivyo vinaweza kuwa vingi masikioni pa Mungu pale ambapo Damu zitaanza kuzungumza kutokea Mavumbini, huku pia vilio vikali vikitokea kutoka kwenye vinywa vya wajane na yatima walioachwa na kunyimwa haki ya kuwa na wazazi wao ambao wanajua wamekatishwa uhai wao kikatili na kwa maonezi. Mungu anaweza kujibu Mapigo na ikawa balaa kwelikweli kwa wahusika wote.
Watanzania Tujizuie kumwaga Damu zisizo na hatia kwa kila njia na kila mbinu iwezekanavyo.Tusiue mtu yeyote yule asiye na hatia.iwe ni kwa imani za kishirikina au chuki binafsi au kutumiwa na watu au kwa malipo ya pesa au kwa kutafuta utajiri au kwa kulipa kisasi au visasi au kukomeshana au wivu tu na mengine mengi ya aina hiyo.
Michael Kalinga Amepigana vita vilivyo vizuri, Mwendo Ameumaliza na Imani Ameilinda.