Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammedi Kawaida akiwa amebeba Jeneza lenye Mwili wa Michael Kalinga

Kwa pamoja tukemee mauaji ya watu wasio na hatia

Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Kutofautiana kifikra sio kosa. Ila siku hizi watu wengine mpaka wanaishia kuuana au kuuwawa. Na kibaya ni kama wanaoua hawakamatiki. Unajiuliza kulikoni?

Nawapa pole wafiwa. Nimesoma mahali kifo chake kinahusiana na mambo ya biashara. Ila wote wanaofanya uuaji lazima washughulikiwe ipasavyo.

Hii sio jamii ya wauaji. Haya mambo yametokea wapi na kama yanazidi kuongezeka
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohammedi Kawaida .Kwa uchungu,maumivu,simanzi ,majonzi na huzuni isiyopimika wala kuelezeka.

Ameshiriki na kuhusika katika shughuli zote za kuaga na kuupumzisha Mwili wa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Machinjioni Makongorosi wilayani Chunya Mkoani Mbeya, Marehemu Michael Kalinga katika Nyumba yake ya Milele.alipoteza Maisha kutokana na kuuwawa kikatili na baadaye Mwili wake kutelekezwa.

Ambapo Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ameweza kubeba Mabegani pake Jeneza Lenye Mwili wa Marehemu Michael Kalinga ambaye kwa sasa Ametangulia Mbele za Haki.

Kwa hakika kifo kinaumiza sana na wala hakizoeleki hata kidogo,hasa pale ambapo kifo hicho kimetokana na kukatishwa uhai na watu wenye roho za kishetani na waliojaa ushetani ndani yao. Kwa hakika Watanzania wote hatuna budi kukemea vikali sana matukio ya namna hii bila kujali itikadi zetu za kisiasa.. Ni lazima tukatae kabisa kumwagilia ardhi yetu kwa Damu zisizo na hatia.

Kwa sababu Damu ya mtu inazungumza hata kama mdomo na kinywa chake kimefumba.Kwa hiyo Damu zisizo na Hatia zikianza kuzungumza na kulia kwa wingi kutoka Mavumbini zilipomwagwa kuelekeza kilio chake machoni, usoni na masikioni pa Mwenyezi Mungu .Basi inaweza kuleta dhahama kutoka kwa Mungu Mwenyewe pale atakapoamua kusikiliza Madai na kilio cha Damu hizo zilizomwagwa Bila Hatia.

Vilio hivyo vinaweza kuwa vingi masikioni pa Mungu pale ambapo Damu zitaanza kuzungumza kutokea Mavumbini, huku pia vilio vikali vikitokea kutoka kwenye vinywa vya wajane na yatima walioachwa na kunyimwa haki ya kuwa na wazazi wao ambao wanajua wamekatishwa uhai wao kikatili na kwa maonezi. Mungu anaweza kujibu Mapigo na ikawa balaa kwelikweli kwa wahusika wote.

Watanzania Tujizuie kumwaga Damu zisizo na hatia kwa kila njia na kila mbinu iwezekanavyo.Tusiue mtu yeyote yule asiye na hatia.iwe ni kwa imani za kishirikina au chuki binafsi au kutumiwa na watu au kwa malipo ya pesa au kwa kutafuta utajiri au kwa kulipa kisasi au visasi au kukomeshana au wivu tu na mengine mengi ya aina hiyo.

Michael Kalinga Amepigana vita vilivyo vizuri, Mwendo Ameumaliza na Imani Ameilinda.

Sawa tu yaani
Mbona yule mgombea wa chadema manyoni alifuatwa nyumbani kwake na kupigwa risasi kiunoni alizikwa?
Yule wa Gongolamboto tuliambiwa alikufa kwa pressure kazikwa.
Yule wa songwe ?
Ben sanane yupo wapi?
Alphoso Mawazo yupo wapi?
Anzory gwanda yupo wapi?
Deo soka yupo wapi?
Wale walikuwa binadamu kama wewe na mimi na walivyokufa ndugu jamaa na marafiki waliambulia kejeli na michbo tu.
 
Nimebubujikwa mimi, ila tulisha ambiwa kifo ni kifo tu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohammedi Kawaida .Kwa uchungu,maumivu,simanzi ,majonzi na huzuni isiyopimika wala kuelezeka.

Ameshiriki na kuhusika katika shughuli zote za kuaga na kuupumzisha Mwili wa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Machinjioni Makongorosi wilayani Chunya Mkoani Mbeya, Marehemu Michael Kalinga katika Nyumba yake ya Milele.alipoteza Maisha kutokana na kuuwawa kikatili na baadaye Mwili wake kutelekezwa.

Ambapo Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ameweza kubeba Mabegani pake Jeneza Lenye Mwili wa Marehemu Michael Kalinga ambaye kwa sasa Ametangulia Mbele za Haki.

Kwa hakika kifo kinaumiza sana na wala hakizoeleki hata kidogo,hasa pale ambapo kifo hicho kimetokana na kukatishwa uhai na watu wenye roho za kishetani na waliojaa ushetani ndani yao. Kwa hakika Watanzania wote hatuna budi kukemea vikali sana matukio ya namna hii bila kujali itikadi zetu za kisiasa.. Ni lazima tukatae kabisa kumwagilia ardhi yetu kwa Damu zisizo na hatia.

Kwa sababu Damu ya mtu inazungumza hata kama mdomo na kinywa chake kimefumba.Kwa hiyo Damu zisizo na Hatia zikianza kuzungumza na kulia kwa wingi kutoka Mavumbini zilipomwagwa kuelekeza kilio chake machoni, usoni na masikioni pa Mwenyezi Mungu .Basi inaweza kuleta dhahama kutoka kwa Mungu Mwenyewe pale atakapoamua kusikiliza Madai na kilio cha Damu hizo zilizomwagwa Bila Hatia.

Vilio hivyo vinaweza kuwa vingi masikioni pa Mungu pale ambapo Damu zitaanza kuzungumza kutokea Mavumbini, huku pia vilio vikali vikitokea kutoka kwenye vinywa vya wajane na yatima walioachwa na kunyimwa haki ya kuwa na wazazi wao ambao wanajua wamekatishwa uhai wao kikatili na kwa maonezi. Mungu anaweza kujibu Mapigo na ikawa balaa kwelikweli kwa wahusika wote.

Watanzania Tujizuie kumwaga Damu zisizo na hatia kwa kila njia na kila mbinu iwezekanavyo.Tusiue mtu yeyote yule asiye na hatia.iwe ni kwa imani za kishirikina au chuki binafsi au kutumiwa na watu au kwa malipo ya pesa au kwa kutafuta utajiri au kwa kulipa kisasi au visasi au kukomeshana au wivu tu na mengine mengi ya aina hiyo.

Michael Kalinga Amepigana vita vilivyo vizuri, Mwendo Ameumaliza na Imani Ameilinda.

Yule mwanamama ccm iringa kuingozi waliyomua kwa kumpiga
Wauaji wamekamatwa au

Ova
 
Back
Top Bottom