Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammedi Kawaida akiwa amebeba Jeneza lenye Mwili wa Michael Kalinga

Kifo cha ali kibao au utekwaji wa dev soka na huu wa juzi wa abdul nondo mbn sijaona makala yako hapa jukwaani.
 
Ungewashauri ndugu zako kwanza
 
Mimi naguswa na vifo vya watu wote wanao uwawa bila hatia .ndio maana nasema tukemee na kulaani vitendo hivyo na kulitaka jeshi la polisi kuwasaka waliohusika.huku sisi watanzania tukitoa ushirikiano kwa jeshi letu.
Nitajie mmoja aliyeuwawa kwa kuwa na hatia.
 
Nitajie mmoja aliyeuwawa kwa kuwa na hatia.
Mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kutoa hukumu na kusema mtu huyu kutokana na makosa haya na haya yaliyothibitishwa bila kuacha shaka ya aina yoyote ile anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
 
Komeni machoko nyie
 
Kuna vifo vya wanasiasa wengine vinauma lakini ila vya wengine haviumi (wapinzani) mahala tumefika ni pabaya sana sisi ni ndugu Kwanini tutoane uhai kisa siasa? Inasikitisha sana
 
Mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kutoa hukumu na kusema mtu huyu kutokana na makosa haya na haya yaliyothibitishwa bila kuacha shaka ya aina yoyote ile anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Sijawahi kuona uzi wako ukilaani mauaji ya watu wasio na hatia ya Mzee Kibao, au yale ya juzi wakati wa uchafuzi wa TAMISEMI.
 
Uhai wa Mwana CCM una thamani zaidi ya yule asiye mwana ccm, au unsemaje Kiongozi Lucas.?
 
Watanzania tuhakikishe ya kuwa itikadi za kisiasa hazitugawi na kuanza kufurahia vifo vya watu vinapotokea kwa kuangalia na kutanguliza uchama .tusifike hatua ya kusema huyu ni wa kwetu na huyu hatuhusu
analeta mpasuko na nani kama si vyombo vyenye dhamana? Na wana siasa wa upande wenu?
Mara ngapi upinzani wanafanyiwa matukio ya kinyama wanalalamika ila hawasikilizwi, akiguswa wenu mna tafuta huruma?
 
Hapa DAR mateja na vibaka hudai swawabu zao huzipata kwenye kubeba majeneza ukipita msafara wa mazishini

Malaria 2 tupe Aya ya Quran
 
Hapa DAR mateja na vibaka hudai swawabu zao huzipata kwenye kubeba majeneza ukipita msafara wa mazishini

Malaria 2 tupe Aya ya Quran
Waislam tunatakiwa tushiriki kikamilifu kushuriki mazishi za Waislamu we zetu kuna fadhila kubwa.
Mtume Muhammad (SAW) amesema:

"Muislamu ana haki tano juu ya ndugu yake: kujibu salamu, kumtembelea mgonjwa, kushirikiana kwenye jeneza lake, kuitikia mwaliko, na kumtakia dua yule anayepiga chafya."
(Bukhari, Hadithi 1240; Muslim, Hadithi 2162)

KUHUSU VIBAKA KUBEBA JENEZA KAMA NDUGU ULIVYOTAKA HILO SINA UJUZI NALO SANA. WALLAH AAALAM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…