Mwenyekiti wa walimu wasio na ajira (NETO) aachiwa kwa dhamana kwa shtaka la kujihusisisha na jumuiya isiyo na usajili

Mwenyekiti wa walimu wasio na ajira (NETO) aachiwa kwa dhamana kwa shtaka la kujihusisisha na jumuiya isiyo na usajili

Gifted fool...
Kuna fani gani Tanzania inaandaliwa kwa ushindani?

Tanzania hii ambao maengeneer wanashindwa hata kutengeneza vitu vidogo vidogo tunaagiza nje?

Nchi hii ambao Kuna wafamasia na wakemia wengi ila hadi Panadol tunaagiza nje?

Halafu elewa interview ya walimu ni complicated, kumbuka elimu ya Tanzania ni nadharia nyingi

Kama mwalimu aanze kudesa kuanzia O level hadi chuo

Unafikiri ni rahisi?


Halafu mtihani wenyewe ni multiple choice maswali 25 tu


Yaani usome kuanzia O level hadi chuo kwa ajili ya kujibu multiple choice? Lazima iwe ngumu ukizingatia watu washaacha Habari za kitaaluma kitambo.

Mimi binafsi nina background nzuri kitaaluma ila kwa mitihani hii ni kubeti tu
 
Ubaya wnafanya watu, na ubaya hulipwa watu. Hakuna kudumu🙏
 
Hawa NETO ni MATOKEO ya elimu mbovu tuliyo nayo ukweli mchungu ni kwamba zaidi ya 90,% ya kada ya ualimu hawakuandaliwa kiushindani katika soko la ajira. Leo wanaona wanaonewa wakati Kuna maelf ya watu wamesoma HR, Gas engineering, petroleum engineering, socialogy nk wako mtaani wanapambana kila siku na bahasha BILA mafanikio.

ENDAPO SERIKALI itakubali KUWEPO Kwa VIKUNDI hivi visivyo Rasmi ni SWALA LA muda vitaanza kutumika kiuanaharakati na madhara yake ni MAKUBWA.

Lazima ifike mahali tukubali haipo SERIKALI inayoweza kumudu ajira Kwa 100%, HAIPO. kujifanya wao ni muhimu sana Kwa JAMII sio sawa. Zipo kada nyingi zinastrugle kila kukicha na hawajaonesha mihemko hii ya kutoka misuli wakati WA kuongea....

Emagine KATIBU ni mwalimu anamfundisha mwanao shuleni. Private sekta usaili Kwa mwalimu ni kawaida kabisaaaaa Kwa sababu Wanataka kilichobora.

Na hawatafikia LENGO lao Kwa sababu SERIKALI haiwezi kuwaajiri WOTE... HAIWEZI HATA ARDHI IPASUKE HUU NDO UKWELII.
Ila serikali inachoweza ni kuongeza posho na mishahara ya wabunge.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Paulo Kaheza, amepewa dhamana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita baada ya kushikiliwa kwa upelelezi kuhusu ushiriki wake katika jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NETO tarehe 25 Februari 2025, Kaheza alikamatwa mnamo 24 Februari 2025 na baadaye kuachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.

NETO imeishukuru jamii ya wanasheria, mashirika ya haki za binadamu kama THRDC na TLS, pamoja na vyombo vya habari na watu wote waliounga mkono juhudi za kuhakikisha kiongozi wao anaachiwa.

Aidha, NETO imesisitiza kuwa si chama cha siasa na hakihusiani na migomo yoyote, bali ni jukwaa la walimu wasio na ajira kushirikiana kupitia mitandao ya kijamii. Umoja huo umesisitiza kwamba utaendelea kuishinikiza serikali kutoa ajira kwa walimu waliomaliza mafunzo yao kati ya mwaka 2015 na 2023, kutokana na uhitaji mkubwa wa walimu mashuleni.

"Tuna matumaini kuwa maombi yetu yatafanyiwa kazi kwa wakati," amesema Daniel Edgar Mkinga, Katibu Mkuu wa NETO, akihitimisha taarifa hiyo.

Ujumbe kutoka kwa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)



Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba Umma haujawahi kushindwa jambo lolote lile pale umma huo unapoamua kwa dhati kabisa ya mioyo yao kutekeleza jambo hilo.

Rejea yale machafuko yaliyotokea katika nchi za kiArab kati ya Mwaka 2011 hadi 2015 kule Tunisia, Libya, Misri, n.k.
Mlipuko wa Vuguvugu lile hatari ulianzia nchini Tunisia, sababu zikiwa ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Rejea pia kule nchini Bangladesh, Mwaka jana wa 2024 Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hasinna lilimkuta jambo huko nchini Bangladesh hadi akalazimika kuokoa nafsi na kukimbilia nchini India, hadi leo hii tunapojadili suala hili bado yupo huko India. Sababu ya yote haya ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.

Aidha, hata mlipuko wa Generation Z kwa majirani zetu wa hapo Kenya, sababu ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

Hivyo Basi, suala hili la Ukosefu wa Ajira kwa Vijana MUST BE HANDLED WITH GREAT CARE!
The Regime of this country Must be very careful in dealing with this Problem of the Youth Unemployment.
Matumizi ya nguvu kubwa hayana nafasi kwenye suala la Utatuzi wa tatizo hili, badala yake AKILI KUBWA, HEKIMA na BUSARA ndiyo silaha sahihi zinazopaswa kutumika katika kutatua Mgogoro huu.
 
Back
Top Bottom