Mwenyekiti wa walimu wasio na ajira (NETO) aachiwa kwa dhamana kwa shtaka la kujihusisisha na jumuiya isiyo na usajili

Gifted fool...
Kuna fani gani Tanzania inaandaliwa kwa ushindani?

Tanzania hii ambao maengeneer wanashindwa hata kutengeneza vitu vidogo vidogo tunaagiza nje?

Nchi hii ambao Kuna wafamasia na wakemia wengi ila hadi Panadol tunaagiza nje?

Halafu elewa interview ya walimu ni complicated, kumbuka elimu ya Tanzania ni nadharia nyingi

Kama mwalimu aanze kudesa kuanzia O level hadi chuo

Unafikiri ni rahisi?


Halafu mtihani wenyewe ni multiple choice maswali 25 tu


Yaani usome kuanzia O level hadi chuo kwa ajili ya kujibu multiple choice? Lazima iwe ngumu ukizingatia watu washaacha Habari za kitaaluma kitambo.

Mimi binafsi nina background nzuri kitaaluma ila kwa mitihani hii ni kubeti tu
 
Ubaya wnafanya watu, na ubaya hulipwa watu. Hakuna kudumu🙏
 
Ila serikali inachoweza ni kuongeza posho na mishahara ya wabunge.
 


Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba Umma haujawahi kushindwa jambo lolote lile pale umma huo unapoamua kwa dhati kabisa ya mioyo yao kutekeleza jambo hilo.

Rejea yale machafuko yaliyotokea katika nchi za kiArab kati ya Mwaka 2011 hadi 2015 kule Tunisia, Libya, Misri, n.k.
Mlipuko wa Vuguvugu lile hatari ulianzia nchini Tunisia, sababu zikiwa ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Rejea pia kule nchini Bangladesh, Mwaka jana wa 2024 Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hasinna lilimkuta jambo huko nchini Bangladesh hadi akalazimika kuokoa nafsi na kukimbilia nchini India, hadi leo hii tunapojadili suala hili bado yupo huko India. Sababu ya yote haya ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.

Aidha, hata mlipuko wa Generation Z kwa majirani zetu wa hapo Kenya, sababu ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

Hivyo Basi, suala hili la Ukosefu wa Ajira kwa Vijana MUST BE HANDLED WITH GREAT CARE!
The Regime of this country Must be very careful in dealing with this Problem of the Youth Unemployment.
Matumizi ya nguvu kubwa hayana nafasi kwenye suala la Utatuzi wa tatizo hili, badala yake AKILI KUBWA, HEKIMA na BUSARA ndiyo silaha sahihi zinazopaswa kutumika katika kutatua Mgogoro huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…