Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.
Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao
Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) Daniel Edigar Mkinga ametangaza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, Joseph Paulo Kaheza akiwa mkoani Geita kwa kile alichodai ni vuguvugu la kupigania ajira kwa walimu wa Tanzania. Ameeleza kuwa alikamatwa na askari hao wakiwa na "silaha kali".
Akizungumza na Jambo TV Jumatatu jioni, Mkinga amesema Joseph amekamatwa mchana wa siku ya Jumatatu mkoani humo katika wakati ambao umoja huo umekubali mwaliko wa kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini.
"Askari hao wameahidi kukamata viongozi wote wa NETO nchini jambo ambalo tunalilaani vikali kwani sisi sio waahini, ni watoto wa kimasikini tunaoiomba serikali haki yetu ya ajira kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri huku mtaani", ameeleza Katibu Mkuu huyo huku akilaani na kuonesha kusikitishwa kwa Joseph kunyimwa dhamana.
Jambo TV imemtafuta Barnabas Daud, ndugu wa Joseph, mkazi wa kata ya Nyankumbu Geita Mjini ambaye ameeleza kuwa Joseph alikamatwa majira ya saa 9 mchana katika mazingira ya kutatanisha kwani awali alimuacha dukani akiwa na mkewe lakini aliporudi hakumkuta. Hata hivyo baadaye gari lisiloonesha waliomo ndani lilifika dukani hapo na watu ambao hawakujitambulisha kama ni askari kutokana na kutoonesha vitambulisho wala kuvaa sare, wakiwa wamemshikilia Joseph kwa pingu mkononi.
Daud anaeleza kuwa miongoni mwa watu wale kuliwapo aliyemfahamu kuwa ni askari, na alipoulizia kosa la nduguye hakuambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa Joseph atapelekwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) na kupewa mawasiliano ya mmoja wa wale wati. Baadaye gari hilo liliondoka na Barnabas akachukua hatua ya kwenda ofisi ya RCO ambako huko aliambiwa nduguye hayupo, akafuatilia kituo kingine cha wilaya ambako hakumkuta, ndipo akawasiliana na askari wa namba aliyoichukua ambaye alimsisitizia kuwa nduguye yupo kwa RCO akihojiwa.
Barnabas alifika kwa RCO saa 11 jioni ambapo aliambiwa arudi saa mbili usiku, aliporudi akakutana na ndugu yake ambaye alimwambia sababu ya kukamatwa kwake ni kuwa sehemu ya kundi la NETO.