Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.

Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) Daniel Edigar Mkinga ametangaza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, Joseph Paulo Kaheza akiwa mkoani Geita kwa kile alichodai ni vuguvugu la kupigania ajira kwa walimu wa Tanzania. Ameeleza kuwa alikamatwa na askari hao wakiwa na "silaha kali".

Akizungumza na Jambo TV Jumatatu jioni, Mkinga amesema Joseph amekamatwa mchana wa siku ya Jumatatu mkoani humo katika wakati ambao umoja huo umekubali mwaliko wa kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini.

"Askari hao wameahidi kukamata viongozi wote wa NETO nchini jambo ambalo tunalilaani vikali kwani sisi sio waahini, ni watoto wa kimasikini tunaoiomba serikali haki yetu ya ajira kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri huku mtaani", ameeleza Katibu Mkuu huyo huku akilaani na kuonesha kusikitishwa kwa Joseph kunyimwa dhamana.

Jambo TV imemtafuta Barnabas Daud, ndugu wa Joseph, mkazi wa kata ya Nyankumbu Geita Mjini ambaye ameeleza kuwa Joseph alikamatwa majira ya saa 9 mchana katika mazingira ya kutatanisha kwani awali alimuacha dukani akiwa na mkewe lakini aliporudi hakumkuta. Hata hivyo baadaye gari lisiloonesha waliomo ndani lilifika dukani hapo na watu ambao hawakujitambulisha kama ni askari kutokana na kutoonesha vitambulisho wala kuvaa sare, wakiwa wamemshikilia Joseph kwa pingu mkononi.

Daud anaeleza kuwa miongoni mwa watu wale kuliwapo aliyemfahamu kuwa ni askari, na alipoulizia kosa la nduguye hakuambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa Joseph atapelekwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) na kupewa mawasiliano ya mmoja wa wale wati. Baadaye gari hilo liliondoka na Barnabas akachukua hatua ya kwenda ofisi ya RCO ambako huko aliambiwa nduguye hayupo, akafuatilia kituo kingine cha wilaya ambako hakumkuta, ndipo akawasiliana na askari wa namba aliyoichukua ambaye alimsisitizia kuwa nduguye yupo kwa RCO akihojiwa.

Barnabas alifika kwa RCO saa 11 jioni ambapo aliambiwa arudi saa mbili usiku, aliporudi akakutana na ndugu yake ambaye alimwambia sababu ya kukamatwa kwake ni kuwa sehemu ya kundi la NETO.
Waliomtuma Sasa wakamtoe maana alikuwa anatafuta kiki za Kisiasa.

Serikali haijiri watu Kwa sababu wamesoma Bali inaajiri Kwa mahitaji na uwezo wa kuwalipa.

Alivyo kiasi eti hataki hata kufanya usaili.kisa alipewa cheti.

Hawa ndio wale walipata div.3
 
Wewe chawa tulia. Hii movement ipo Hadi vijijini kabisa Sasa elewa kuwa mabadiliko ya mfumo yanahitajika. Lazima tule wote cake ya taifa hili Kwa haki na Kwa usawa. Si kikundi Cha watu wachache ndiyo waendelee kunufaika na cake ya taifa Kwa kisingizio eti serikali haiwezi/haiajiri Kwa sababu umehitimu ila tu Kwa mahitaji. Ma CCM uwezo wenu unaishia hapo ndiyo maana mnataka wananchi wote tuwe wanaharakati.
 
Nchini Zaire (DRC)! ilikuwa ni Kosa kubwa sana kwa kufanya Kitendo cha Kumkosoa mtawala wa nchi hiyo Dikteta Mobutu Sese Seko au kuukosoa Utawala wake. Hali ipo hivyo pia nchini Urusi kwa Putin na nchini China.

Kuwakosoa Madikteta ni sawa sawa na kujikatia tiketi ya kifo.
Mholand umeibania habari.
 
Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.

Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) Daniel Edigar Mkinga ametangaza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, Joseph Paulo Kaheza akiwa mkoani Geita kwa kile alichodai ni vuguvugu la kupigania ajira kwa walimu wa Tanzania. Ameeleza kuwa alikamatwa na askari hao wakiwa na "silaha kali".

Akizungumza na Jambo TV Jumatatu jioni, Mkinga amesema Joseph amekamatwa mchana wa siku ya Jumatatu mkoani humo katika wakati ambao umoja huo umekubali mwaliko wa kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini.

"Askari hao wameahidi kukamata viongozi wote wa NETO nchini jambo ambalo tunalilaani vikali kwani sisi sio waahini, ni watoto wa kimasikini tunaoiomba serikali haki yetu ya ajira kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri huku mtaani", ameeleza Katibu Mkuu huyo huku akilaani na kuonesha kusikitishwa kwa Joseph kunyimwa dhamana.

Jambo TV imemtafuta Barnabas Daud, ndugu wa Joseph, mkazi wa kata ya Nyankumbu Geita Mjini ambaye ameeleza kuwa Joseph alikamatwa majira ya saa 9 mchana katika mazingira ya kutatanisha kwani awali alimuacha dukani akiwa na mkewe lakini aliporudi hakumkuta. Hata hivyo baadaye gari lisiloonesha waliomo ndani lilifika dukani hapo na watu ambao hawakujitambulisha kama ni askari kutokana na kutoonesha vitambulisho wala kuvaa sare, wakiwa wamemshikilia Joseph kwa pingu mkononi.

Daud anaeleza kuwa miongoni mwa watu wale kuliwapo aliyemfahamu kuwa ni askari, na alipoulizia kosa la nduguye hakuambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa Joseph atapelekwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) na kupewa mawasiliano ya mmoja wa wale wati. Baadaye gari hilo liliondoka na Barnabas akachukua hatua ya kwenda ofisi ya RCO ambako huko aliambiwa nduguye hayupo, akafuatilia kituo kingine cha wilaya ambako hakumkuta, ndipo akawasiliana na askari wa namba aliyoichukua ambaye alimsisitizia kuwa nduguye yupo kwa RCO akihojiwa.

Barnabas alifika kwa RCO saa 11 jioni ambapo aliambiwa arudi saa mbili usiku, aliporudi akakutana na ndugu yake ambaye alimwambia sababu ya kukamatwa kwake ni kuwa sehemu ya kundi la NETO.
Waziri MSOMI kasema anataka akutane nao,ombi,Afande kakamata,Amri!! Duuh
 
Sasa mbona huna akili kama siyo kweli?
Akili zipi wewe mzee! Ni kukariri tu kwamba lazima uajiriwe ndo utoke kimaisha mimi nipo nakomaa bajaji ya mkataba na Ninaishi boss,

Na bado ninajifua na kwenye u-mechanic uhakika wa kupata magari vimeo upo hukosi 10-15k kama ni fundi MUAMINIFU
 
Wewe chawa tulia. Hii movement ipo Hadi vijijini kabisa Sasa elewa kuwa mabadiliko ya mfumo yanahitajika. Lazima tule wote cake ya taifa hili Kwa haki na Kwa usawa. Si kikundi Cha watu wachache ndiyo waendelee kunufaika na cake ya taifa Kwa kisingizio eti serikali haiwezi/haiajiri Kwa sababu umehitimu ila tu Kwa mahitaji. Ma CCM uwezo wenu unaishia hapo ndiyo maana mnataka wananchi wote tuwe wanaharakati.
Hakuna serikali inayogawa pesa Wala kuajiri watu Ili iqatoe kwenye njaa na jobless.

Serikali ikiamua kuwasaka Iliweza na mkapoteana.

Mlikuwa wapi kuunda hicho kiumoja chenu za Kisiasa awamu ya Magufuli ambae alikuwa haajiri ndio mje kuleta ujinga wenu awamu ya mama aliyewaonea huruma?

By the way nyie mbumbumbu mnaotumika mlipata div.3 harafu hamtaki Usaili eti mna vyeti 😂😂
 
Kunyimwa dhamans kuna sababu nyingi ila za moja kwa moja huwa ni ama hajakamatwa kwa kosa lolote, hapo hawezi kupewa dhamana sababu hana kosa alilokamatwa nalo.

Sababu nyingine inaweza ikawa kwa ajili ya kuulinda usalama wake yeye mwenyewe. Baada ya intelijensia ya polisi kuona ipo hiyo sababu.

Sasa usiniulize mtu anakamatwaje bila kosa, hilo linawezekana na limeruhusiwa na sheria zetu wenyewe. Kukamatwa sio kosa kosa ni lile lililofanyika tu.
Hii Sheria yavkukamatwa Halafu hupewi dhamana ni mbovu kabisa!
 
Hakuna serikali inayogawa pesa Wala kuajiri watu Ili iqatoe kwenye njaa na jobless.

Serikali ikiamua kuwasaka Iliweza na mkapoteana.

Mlikuwa wapi kuunda hicho kiumoja chenu za Kisiasa awamu ya Magufuli ambae alikuwa haajiri ndio mje kuleta ujinga wenu awamu ya mama aliyewaonea huruma?

By the way nyie mbumbumbu mnaotumika mlipata div.3 harafu hamtaki Usaili eti mna vyeti 😂😂
Ila kwenye usaili wamefeli mwalimu ni mwalimu! Ni kama dereva lazima ujifunze Kila siku
 
Kwanza mtaala Mpya wamepiga marufuku kusomesha watu vilaza wa divi.3 kuwa walimu.

Hiyo iende Hadi kwenye Afya wanakoweka vilaza wa D.

Hizo fani hazihitaji watu wenye akili ndogo kama Hawa wanaodai kwamba Kwa kuwa wamepata vyeti wasifanye Usaili 😂😂
 
Akili zipi wewe mzee! Ni kukariri tu kwamba lazima uajiriwe ndo utoke kimaisha mimi nipo nakomaa bajaji ya mkataba na Ninaishi boss,

Na bado ninajifua na kwenye u-mechanic uhakika wa kupata magari vimeo upo hukosi 10-15k kama ni fundi MUAMINIFU
Hao walimu walisoma ili wajiajiri?
 
Publicity without thinking about the current situation, hapo ngoja awe mfano.

huyu nahisi ni mwana jf aka ona apite na upepo, haya hao member wa neto wampambanie Sasa.
Mtu anatetea anachokiamini wewe unaona anatafuta publicity, chochote tu kitakachomtokea maisha yataendelea
 
Back
Top Bottom