Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Rogie

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
7,586
Reaction score
6,697
Manji.jpg

Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .

Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.

Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.

Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .

Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.

Chanzo: Shaffih Dauda

Updates 16.08.2016 Saa 5 dk 41 asubuhi.

Kikao cha viongozi wa Matawi ya Klabu ya Yanga kimemsimamisha Mzee Akilimali baada ya kauli ya Mzee Akilimali kusemekana kumkashifu Manji kuwa "Amekurupuka".

"Katika watu tunaompenda Manji mimi ni namba moja na namba mbili"- Mzee Akilimali

"Mwana umleavyo ndio akuavyo, Manji alikuwa anatuita akitaka kufanya jambo ila siku hizi hatuambii lolote"- Mzee Akilimali

"Nimemwambia Mr Manji na mimi nimempa Uchifu wa Yanga, sisi tunampenda kweli Yusuf na nimemtaka radhi jana" - Mzee Akilimali

"Kama kukurupuka ni tusi kama nilivyomwambia Yusuf basi namba radhi kwake na WanaYanga wote" - Mzee Akilimali
 
Habari zinazosambaa mitaani ni kuwa Mwenyekiti wa Yanga kaamua kubwaga manyanga mara baada ya kuchoshwa na matusi ya matajiri wengine kisa yeye kuikodisha yanga miaka 10

"Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni wapenzi wa Yanga. . Hawapendi mimi niwepo pale. . Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa klabu yangu. . Kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote?najiuzulu". . Ni kauli ya mwenyekiti wa Yanga SC ambaye ametangaza kujiuzulu kufuatia kusakamwa na hasa baada ya kuomba kuichukua Yanga kwa miaka 10.

Hata hivyo kumekuwa na vikao mbalimbali kumsihi Manji abadili maamuzi yake lakini inaonekana amechoka na ameamua kuibwaga Yanga.Tayari Reginald Mengi ameonesha nia ya kuingia Yanga endapo Manji ataondoka. . Leo jioni baraza la wazee wanataraji kuwa na kikao na Mengi.

Tusubiri.

=======

TAARIFA ZAIDI..

Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.

“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.

Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.

“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari.
 
Bado ni tetesi
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.

“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."
 
Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .
Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.
Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .

Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.
He is childish anapenda kuabudiwa na kusujudiwa, Kama Ana njia njema Kwa nini anashindwa ku argue his case? Watanzania watakua ma mbumbumbu kutoa time ya wananchi waliojenga tangu Uhuru Kwa hiyo hela kiduchu. Tuliwashangaa wana yanga Kwa nini anataka nembo Kubwa hivyo for only 500per annum? Hiyo ni budget ndogo sana Kwa nembo inayo mean lives Za watu vizazi Kwa vizazi. Why 75% why not 51% or 49% Kama kweli anataka uzalendo?
 
Ni jambo la ajabu maamuzi ya wengi yanaonekana eti hawana akili wamekurupuka kuliko mzee na wenzie walieshindwa kufanya chochote ndani ya Yanga kwa wakati wote waliokuwepo pale zaidi ya kuganga njaa na wengine kushindwa kutia chochote, lakini mzee ni mnafiki sana sijui safari hii hajapewa chochote maana ndio huwa mtetezi mkuu leo kageuka kawa Yuda kwa Mwenyekiti, wazee wa nana hii ni hatari sana kwa jamii.
 
He is childish anapenda kuabudiwa na kusujudiwa, Kama Ana njia njema Kwa nini anashindwa ku argue his case? Watanzania watakua ma mbumbumbu kutoa time ya wananchi waliojenga tangu Uhuru Kwa hiyo hela kiduchu. Tuliwashangaa wana yanga Kwa nini anataka nembo Kubwa hivyo for only 500per annum? Hiyo ni budget ndogo sana Kwa nembo inayo mean lives Za watu vizazi Kwa vizazi. Why 75% why not 51% or 49% Kama kweli anataka uzalendo?

Unajielewa kweli wewe, mambo ya Yanga yanakuhusu nini au ulisahau kuja kuwashangilia wale waarabu
 
Back
Top Bottom