Monday, August 15, 2016
Kauli ya Manji baada ya taarifa kwamba amejitoa Yanga

Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu uenyekiti kuzagaa,Manji alitafutwa kuelezea tetesi hizo.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.
“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."
Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.
Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.
Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.Walio karibu na Manji wanasema amesikika akilalamika kuwa kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dsm ya hivi karibuni,aliyosema kuwa "Ukitaka kujuwa kwanini Tanzania ni masikini,angalia mkataba watakaosaini Yanga na Manji".Kauli hiyo imeonekana kumshitua Manji na kusema kuwa nyuma ya Makonda kuna viongozi wengi wa serikali ambao hawataki yeye achukuwe timu ya Yanga.
Manji anasema kuwa amepata habari kuwa viongozi wengi wa Serikali wa ngazi z juu hawataki yeye akae Yanga,na viongozi hao wanawatumia Wazee wa Yanga kama Mzee Akilimali na watu kama RC Dsm ili kumtoa katika reli na baadae matajili wengine waichukuwe Yanga.