Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Wewe itakua ni mmoja wa wanaoibomoa yanga au si mshabiki wa yanga, kwani kwa sasa hivi hiyo yanga inafaidika nini na hiyo nembo? Bora nusu hasara kuliko hasara kabisa
 
Hivi na udhamini wake ndio basi tena na Quality Group yake?
 
Usisahau kuwa katika viongozi wa yanga Manji ndo mkuu pale
 
Du, afadhali sasa wanayanga wataendesha klabu yao kwa maslahi ya klabu maana huyu kanji alikuwa amedhamiria kuinyonya yanga kama kupe kwa muda wa miaka 10! Yanga oyeeeeeee!
Mkuu pesa mnayoo au unapiga mayowe tu
 
Wakati nyumbu wa jangwani washanza kushikAna mashati uku upande wa mambo yanayooka tena
 

Attachments

  • 1471289868967.jpg
    53.6 KB · Views: 27
Aisee mbona mnaanza uchawi asubuhi asubuhi.........viongozi wa serikali kwani hicho ni chama cha siasa????
Yanga ni Mhimili wa Nne wa Dola, kuidhibiti ni kazi ya Taifa zima, hawezi kuachiwa mja mmoja.
 
Yaani nyie badala ya kukaa kujiuliza ni lini mtalipa lile deni letu tulipowatandika sita mtungi, bado mnawayawaya wala hamjui njia ya kupita!!
 
Huu ni wakati wetu simba magufuli simba na majaaliwa kassim simba unategemea mambo yatakuwaje?
 


Monday, August 15, 2016
Kauli ya Manji baada ya taarifa kwamba amejitoa Yanga

Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu uenyekiti kuzagaa,Manji alitafutwa kuelezea tetesi hizo.

Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.

“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.

Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.


“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."

Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.

Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.

Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.Walio karibu na Manji wanasema amesikika akilalamika kuwa kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dsm ya hivi karibuni,aliyosema kuwa "Ukitaka kujuwa kwanini Tanzania ni masikini,angalia mkataba watakaosaini Yanga na Manji".Kauli hiyo imeonekana kumshitua Manji na kusema kuwa nyuma ya Makonda kuna viongozi wengi wa serikali ambao hawataki yeye achukuwe timu ya Yanga.

Manji anasema kuwa amepata habari kuwa viongozi wengi wa Serikali wa ngazi z juu hawataki yeye akae Yanga,na viongozi hao wanawatumia Wazee wa Yanga kama Mzee Akilimali na watu kama RC Dsm ili kumtoa katika reli na baadae matajili wengine waichukuwe Yanga.
 
Tumechoka na mikwara yake, kama anasepa asepe
 
Manji ni lazima afahamu Yanga ni klabu ya ccm ingawa na wana UKAWA wapo wanachama, akishalijuwa hili anunuwe timu ya ligi aanzishe timu yake kama alivyofanya Bakhresa.

Hata huko Simba ni yaleyale tu hizi timu waachiwe wenyewe wakaanga sumu tunahitaji TP Mazembe ya Tanzania, ushabiki wa mazoea umeshapitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…